Serikali nchini Mexico imethibitisha kuwa jeshi lake la majini limemkamata kiongozi mkuu wa kundi linalotuhumiwa kufanya biashara ya madawa ya kulevywa. Miguel Angel Trevino Morales, kiongozi wa kundi linalouza madawa ya kulevywa la Zetas , amekamatwa katika mji wa Nuevo Laredo, ambao uko katika mpaka na jimbo la Texas nchini Marekani , pamoja na watu wengine wawili.
Kundi la Zetas liliundwa na wanajeshi wa kikosi maalum na linaonekana kuwa moja kati ya makundi yenye kuongopwa nchini Mexico na yanayofanya uhalifu wa kupangiliwa .
Kukamatwa huko kunaelezwa kuwa ni hatua kubwa iliyopigwa na pigo kubwa kwa makundi yanayofanya biashara ya mihadarati nchini Mexico, ambayo yanahusishwa na ongezeko la matukio ya ghasia na zaidi ya vifo 70,000 tangu mwaka 2006.
Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani imetoa zawadi ya hadi dola milioni tano ili kupata taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa Trevino Morales.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni