Idadi ya vifo katika ajali ya treni nchini Hispania yafikia 77
Habari kutoka kwa ofisa wa eneo la Galicia la Hispania zinasema,
idadi ya watu waliokufa katika ajali ya treni iliyoacha njia imefikia
77.
Waziri mkuu wa Hispania Bw. Mariano Rajoy ametoa salamu za
rambirambi kwa wafiwa katika ajali hiyo, na kuwatakia majeruhi wapone
haraka.
Ajali hiyo ilitokea usiku wa tarehe 24, wakati treni hiyo ilipokuwa ikitoka Madrid na kuelekea eneo la Galicia
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni