Walimu wa shule za umma wa Kenya wamehitimisha mgomo wao uliodumu
kwa kipindi cha wiki 4 baada ya kufikia makubaliano ya awali na
serikali ya nchi hiyo.
Uamuzi huo wa kuhitisha mgomo wa walimu ulitangazwa jana baada ya viongozi wa serikali Kenya kutoa amri ya kufungungwa shule za msingi kwa muda usiojulikana. Baada ya makubaliano hayo ya awali Jumuiya ya Walimu wa Kenya imewataka walimu warejee kazini kuanzia leo Alkhamisi.
Walimu wa Kenya walianza mgomo kote nchini yapata siku 24 zilizopita wakidai marupurupu yao.
Mwezi Aprili mwaka huu Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alitangaza kuwa hali ya sasa ya nchi hiyo hairuhusu kuongezwa mishahara ya walimu na wafanyakazi wa sekta ya umma.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni