Hali ya wasiwasi na taharuki inaendelea kutanda nchini Tanzania baada ya kuenea habari za kupigwa risasi Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda usiku wa kuamkia leo. Magazeti ya Tanzania pamoja na mitandao ya kijamii imeripoti kuhusu tukio hilo ingawa haijabainika nini hasa kinachoendelea.
Kwa mujibu wa ripoti za mitandao ya kijamii ni kwamba, Sheikh Ponda alipigwa risasi na polisi huko Morogoro baada ya kutoa mhadhara katika msikiti mmoja mjini hapo. Hata hivyo polisi wamekanusha kumpiga risasi kiongozi huyo wa kidini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni