Jumamosi, 24 Agosti 2013

Mtoto wa miaka 8 amuuwa mlezi wake Marekani


Mtoto wa miaka 8 amuuwa mlezi wake Marekani
Mtoto wa kiume aliye na umri wa miaka minane amemuuwa kwa makusudi kwa kumpiga risasi mlezi wake aliyekuwa na umri wa miaka 90 baada ya kutazama mchezo wa video wenye vitendo vya utumiaji mabavu huko Louisiana nchini Marekani. Mwanamke huyo mlezi aliaga dunia baada ya kupigwa risasi kichwani wakati akitazama televisheni.
Mauaji hayo yalitokea huko Marekani Alhamisi iliyopita na mama huyo mlezi alitajwa kuwa ameaga dunia mara baada ya kupigwa risasi. Polisi imesema kuwa mtoto huyo aliye na umri wa miaka mianne alitenda mauaji hayo baada ya kucheza mchezo wa video kwa jina la "Grand Theft Auto IV", ambao umejaa vitendo vya utumiaji mabavu na ukatili na ambao hutoa pointi kwa wachezaji wanaouwa watu. 
Polisi wamesema kuwa mtoto huyo amewaeleza wachunguzi kuwa alimuuwa mlezi wake huyo kwa bahati mbaya, japokuwa wachunguzi wamesema kuwa ushahidi unaonyesha kwamba alimuuwa bibi huyo kwa makusudi wakati akichezea silaha hai. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni