Jumatano, 18 Septemba 2013

Panasonic kufufua kiwanda chake kilichoko Dar es Salaam.



Kampuni ya Panasonic, imesema inaangalia uwezekano wa kuanza kuzalisha bidhaa za kisasa kwenye kiwanda chake kilichoko Dar es Salaam nchini Tanzania.
Hayo yamefichuliwa na mkurugenzi mkuu wa Panasonic katika eneo la mashariki ya kati na Afrika, Masao Motoki, alipokuwa akizungumza katika maonyesho ya bidhaa zao mpya za kampuni hiyo zinazoendana na mazingira ya Afrika.
Pia alisema ili kuleta ushindani na kuzalisha wataalamu bora, wanaangalia uwezekano wa kushirikiana na vyuo mbalimbali ili wanafunzi waweze kujifunza kuhusu teknolojia mpya.
Kwa mujibu wa Motoki, Tanzania ni nchi ya tatu katika Afrika kwa kununua bidhaa za kampuni hiyo .
Nchi ya kwanza ikiwa ni Kenya ikifuatiwa na nchi ya Nigeria.
Naye mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo barani Asia na Pacific, Yorihisa Shiokawa, anasema bara la Afrika ni soko kubwa la bidhaa mbalimbali linalochipukia kwa kasi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni