Ijumaa, 12 Julai 2013

Malala: Elimu ndiyo suluhisho pekee

Msichana wa Pakistan aliyepigwa risasi na Taliban nchini humo, Malala Yousafzai, amesema kuwa siku ya malala duniani sio kwa ajili yake, bali ni kwa ajili ya wanawake, wasichana na wavulana waliopaza sauti kutetea haki zao. Malala ametoa kauli hiyo leo wakati akihutubia kwa mara ya kwanza katika Baraza Kuu la Vijana la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani. Malala ambaye leo anatimiza miaka 16, alipigwa risasi kichwani na Taliban mwezi Oktoba mwaka uliopita, baada ya kutetea haki ya watoto wa kike kupatiwa elimu. Amesema kuwa silaha kubwa kwao ni vitabu na peni na kwamba elimu ndio suluhisho pekee. Malala amemkabidhi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ombi lililosainiwa na karibu watu milioni nne linalotaka kusaidiwa kwa watoto milioni 57 wasio na uwezo wa kwenda shule pamoja na kuwafadhili walimu, shule na vitabu ili kufikia lengo la elimu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni