Ijumaa, 12 Julai 2013

Waziri afungwa Romania

Mahakama moja nchini Romania, imemuhukumu waziri wa usafiri Relu Fenechiu kifungo cha miaka mitano jela kutokana na rushwa. Fenechiu amepatikana na hatia ya kuuza vifaa vya umeme vya mitumba kwa kampuni ya nchi hiyo kwa gharama za vifaa vipya kati ya mwaka 2002 na 2005. Waendesha mashtaka wamesema kuwa vifaa hivyo viligharimu Euro milioni 1.7. Fenechiu ambaye amekuwa akikanusha madai hayo na kukataa kuachia madaraka, anakuwa waziri wa kwanza wa Romania kupewa adhabu ya kifungo jela. Wakili wake amesema mteja wake atakata rufaa. Kwa mujibu wa sheria za Romania, Fenechieu hatokwenda jela hadi rufaa yake itakaposikilizwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni