Jumanne, 9 Julai 2013

Taarifa zazidi kutolewa ajali ya ndege ya Asiana

Kumekuwepo maelezo zaidi yanayotolewa kuhusiana na ajali ya ndege ya kampuni ya Asiana, iliyoanguka mjini San Francisco nchini Marekani.
Mkuu wa idara ya zimamoto Joanne Hayes-White na naibu mkuu msaidizi Dale Carnes, wote wamezungumzia uwezekano kuwa wasichana wawili waliouawa huenda waligongwa na gari la dharura lililokuwa linawahi eneo la ajali hiyo iliyotokea siku ya Jumamosi.
Wachunguzi wamesema pia kuwa ndege hiyo nambari 214 ilikuwa inakwenda kwa ndogo kuliko kawaida wakati ikikaribia uwanjani hapo, na kwamba marubani walijaribu kuahirisha kutua kabla ndege hiyo haijaanguka katika barabara ya kurukia.
Kampuni ya Asiana ilisema jana mjini Seoul kuwa rubani alikuwa na uzoefu mdogo wa kuendesha ndege ya Boeing 777, na kwamba alikuwa akitua katika uwanja wa kimataifa wa San Francisco kwa mara ya kwanza

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni