Jumamosi, 3 Agosti 2013

Afisa wa Marekani akimbia Kenya baada ya kuua


Maafisa nchini Kenya wamesema kuwa afisa mmoja wa ubalozi wa Marekani nchini humo ambaye alimuua raia mmoja wa Kenya baba wa watoto watatu na kuwajeruhi wengine wanane katika ajali ya gari huko Nairobi, ametoroka nchini humo. Maafisa wa Kenya wameripoti kuwa mwanadiplomasia huyo wa Marekani kwa jina la Johsua Walde alikiuka sheria za barabarani na kugonga gari la abiria aina ya matatu na kuua mtu mmoja na kuwajerhi vibaya abiria wengine wanane Julai 11 mwaka huu. Baada ya kutokea ajali hiyo, maafisa wa ubalozi wa Marekani mjini Nairobi siku iliyofuata walimsafirisha nje ya nchi mwanadiplomasia huyo na familia yake.
Ubalozi wa Marekani mjini Nairobi baadaye ulitoa salamu za rambirambi kwa familia ya mhanga wa ajali hiyo. Hata hivyo haukutaja fidia yoyote utakayotoa kwa familia  hiyo iliyosalia bila ya msaada wowote wa kifedha ili kugharamia shughuli za mazishi na gharama za hospitali kwa majeruhi wengine wa ajali hiyo iliyosababishwa na mwanadiplomasia wao.  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni