Jumamosi, 3 Agosti 2013

JK: Uhusiano wa Tanzania na Rwanda uendelee,,,,,,,


Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania alisema jana kuwa uhusiano wa nchi yake na Rwanda umeharibika kutokana na juhudi zake za kurejesha amani katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia. Akihutubia wananchi katika hotuba yake ya kila mwezi, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema kuwa nchi yake hata hivyo inataka kuendeleza uhusiano wake wa kihistoria na Rwanda huku ikifanya jitihada za kurejesha amani huko Kongo. Tanzania inaongoza kikosi kipya cha uingiliaji kati cha Umoja wa Mataifa huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako waasi wa harakati ya Machi 23, kundi ambalo wengi wa wapiganaji wake ni wa kabila la Watutsi  na ambao kwa kiasi kikubwa wanasadikiwa  kuwa wanaungwa mkono na Rwanda, wamekuwa wakiendesha mapigano dhidi ya jeshi la Kongo na makundi mengine ya waasi mashariki mwa nchi hiyo. Hata hivyo Rwanda imekanusha tuhuma hizo za kuwaunga mkono waasi wa M23. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni