Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu (PAC), Zitto Kabwe.
Na Mwandishi Wetu, Mwananchi
Alisema walipitia mpango wa Serikali na
kugundua kuwa mapato yasiyo ya kikodi yamekadiriwa kuwa ni Sh741 bilioni
kutoka wizara, idara na mikoa.
Taarifa iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati
ya Bunge ya Hesabu (PAC), Zitto Kabwe imesema kwa sasa Serikali
hukusanya Sh741 bilioni kwa mapato yasiyo ya kikodi ambayo ni nusu tu ya
mapato ambayo Serikali ingestahili kupata.
Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini
(Chadema), ameishauri Serikali itumie risiti za elektroniki kwa
kukusanya maduhuli.
“Utaratibu wa kutumia risiti za elektroniki
utaongeza maradufu mapato ya Serikali na kuifanya kuachana na mtindo wa
kupandisha kodi kwenye bidhaa muhimu kwa wananchi.
“Uamuzi wa Kamati za Bunge za Hesabu wa kuitaka
Serikali kukusanya maduhuli yake kwa kutumia risiti za elektroniki
unapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania,” ilisema taarifa hiyo ya
Zitto.
Alisema walipitia mpango wa Serikali na kugundua
kuwa mapato yasiyo ya kikodi yamekadiriwa kuwa ni Sh741 bilioni kutoka
wizara, idara na mikoa.
“Serikali inapata Sh383 bilioni kutoka kwenye
halmashauri za wilaya, miji na manispaa. Hatukuweza kupata mapato ya
mashirika ya umma maana hayaletwi kwenye Bajeti za Serikali,” alisema.
Wizara zinazoongoza kwa mapato (mapato kwenye
mabano ni Nishati na Madini (Sh220 bilioni), Fedha (Sh126 bilioni),
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (Sh100 bilioni), Maliasili na
Utalii (Sh84 bilioni), Mambo ya Ndani (Uhamiaji Sh92 bilioni na Usalama
Barabarani Sh17 bilioni), Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi (Sh19 bilioni),
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (Sh16 bilioni).
Hata hivyo, Zitto alisema mapato ya Serikali yameongezeka kwa asilimia 60 kutoka Sh500 bilioni mpaka Sh800 bilioni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni