Mfanyakazi wa zamani wa shirika la ujasisi la Marekani, CIA, Edward Snowden amesema anataka kuomba hifadhi ya muda nchini Urusi. Snowden aliyatangaza hayo jana mjini katika mkutano na wanaharakati wa haki za binadamu.
Mkutano huo ulifanyika katika sehemu ya wasafiri wa kimataifa katika uwanja wa ndege wa Sheremetyevo, mjini Moscow, ambako amekuwapo kwa muda wa wiki tatu. Mtaalamu huyo wa kompyuta alisema anataka kubakia nchini Urusi hadi pale atakapoweza kwenda Amerika ya Kusini. Marekani imeionya Urusi iache kumpa Snowden kile ilichokiita jukwaa la propaganda.
Jana, Rais Barack Obama wa Marekani alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin. Urusi imekwishatangaza kwamba Snowden ambaye amefichua mpango wa siri wa Marekani kuchunguza mawasiliano ya simu na mitandao ya kimataifa, anaweza kuruhusiwa kubakia nchini humo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni