Rais wa Marekani Barack Obama ameziamuru idara
zinazohusika nchi humo kuangalia upya msaada
unaotolewa na nchi yake kwa serikali ya Misri. Wizara ya
Usalama ya marekani imesema katika taarifa iliyotolewa
jana kuwa Obama amaetoa agizo hilo kutokana na matukio
yaliyotokea nchini Misri wiki iliyopita, lakini haikuzungumzia
moja kwa moja mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa rais
Mohamad Mursi madarakani. Wakati huo, afisa moja nchini
humo, ambae hakutaka jina lake litajwe, amesema mpango
wa marekani kuwasilisha ndege za kivita aina ya F-16 kwa
nchi hiyo katika wiki chache zijazo bado uko palepale licha
ya agizo la rais.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni