Bei ya bia, sigara zazidi kupanda.

Kwa ufupi
Pia bia nyingine zote zimepanda kutoka Sh525 kwa
lita hadi Sh578, sawa na ongezeko la Sh51 kwa lita. Kuhusu ushuru
magari, umeongezwa kwenye magari yasiyozalisha na yenye umri wa miaka 10
kutoka asilimia 20 mpaka hadi asilimia 25.
Bungeni DodomA. Serikali imeendelea kuongeza kodi
kwenye magari makuukuu, bia, vinywaji vikali, na baridi kama ambavyo
kodi imekuwa ikifanya kila mwaka na kuwaathiri watumiaji.
Kutokana na hali hiyo wanywaji pombe na sigara
pamoja na waagizaji magari watalazimika kutumia fedha nyingi zaidi ili
kupata huduma hizo.
Vilevile baadhi ya bidhaa zisizokuwa za mafuta
nazo zimefanyiwa marekebisho na kuongezwa kodi, ikiwamo mvinyo, pombe,
vinywaji vikali, na sigara.
Vinywaji hivyo vimeongezwa kodi kwa asilimia 10.
Kutokana na bajeti ya mwaka 2013/14 iliyosomwa jana bungeni na Waziri wa
Fedha, Dk William Mgimwa, vinywaji vikali vimepanda kutoka Sh2,392 hadi
Sh2,631 kwa lita, sawa na ongezeko la Sh239 kwa lita moja.
Bia inayotengenezwa kwa nafaka nchini ambayo
haijaoteshwa imeongezwa kodi kutoka Sh310 kwa lita hadi Sh341, sawa na
ongezeko la Sh31 kwa lita.
Pia bia nyingine zote zimepanda kutoka Sh525 kwa
lita hadi Sh578, sawa na ongezeko la Sh51 kwa lita. Kuhusu ushuru
magari, umeongezwa kwenye magari yasiyozalisha na yenye umri wa miaka 10
kutoka asilimia 20 mpaka hadi asilimia 25.
Dk Mgimwa alisema hatua hiyo imelenga kupunguza
uagizaji wa magari chakavu ili kulinda mazingira na kupunguza ajali za
mara kwa mara, huku ikiongeza mapato kwa Sh510 bilioni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni