Kundi la Taliban leo limedai kuhusika na shambulio
nchini Afghanistan ambalo limewauwa wanajeshi
wanne wa Marekani ikiwa ni saa chache tu baada ya
serikali ya Marekani kusema itakuwa na
mazungumzo na waasi wa kundi hilo juu ya
kukomesha mzozo uliodumu zaidi ya muongo mmoja
nchini humo. Shambulio hilo la roketi huko Bagram
katika kambi kubwa kabisa ya kijeshi inayoongozwa
na Marekani kaskazini mwa Kabul linaonyesha
usugu wa waasi hao wa itikadi kali ya Kiislamu
ambao mara kwa mara wamekuwa wakifaya
mashambulizi katika vituo muhimu. Kabla ya
shambulio hilo Rais wa Marekani, Barack Obama,
aliyakaribisha mazungumzo na kundi hilo
yaliyopangwa kufanyika Qatar akisema ni hatua
muhimu.
SOURCE---IDHAA YA KISWAHILI
SOURCE---IDHAA YA KISWAHILI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni