Jumatano, 19 Juni 2013

Umoja wa Mataifa wasema idadi ya wakimbizi ni kubwa

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa idadi ya wakimbizi duniani imeongezeka na kufikia milioni 45 idadi ambayo haikuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 18. Ripoti ya Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, iliyotolewa leo hii mjini Geneva, imesema kuongezeka kwa idadi hiyo ya wakimbizi kumechangiwa na mizozo ya Syria, Mali na maeneo mengine ya vurugu barani Afrika. Kwa mujibu wa shirika hilo zaidi ya watu milioni saba na nusu wamelazimika kukimbia nyumba zao mwaka jana. Kiwango hicho kina maana kwamba kila baada za sekunde nne kunakuwepo na mtu anayelazimika kukimbia makaazi yake. Waafghanistan wanaendelea kuwa kundi kubwa lenye wakimbizi nje ya nchi hiyo ambapo hapo mwaka jana walikuwa milioni 2.6 wakifuatiwa na Wasomali, Wairaq, Wasyria na Wasudan.

Makala zetu

Ujerumani na uraia wa nchi mbili

Limekuwa ni suala linaloepukwa sana kwenye mataifa mengi duniani, lakini kuwaruhusu watu kuwa na uraia wa nchi zaidi ya moja kunatajwa kuwa na faida zake.
Oummilkheir na namna Ujerumani inavyolichukulia suala la wananchi kuwa na uraia wa nchi zaidi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni