Bunge la nchi za Kiarabu limelaani mauaji ya kisiasa yaliyotokea huko Tunisia na Libya na kueleza kuwa, utatuzi wa kisiasa ndio njia bora zaidi ya kuhitimisha mgogoro ulioikumba Misri.
Spika wa Bunge la nchi za Kiarabu Ahmad bin al Jarwan ametoa taarifa akilaani vikali kuuawa viongozi wa upinzani huko Tunisia na Libya. Al Jarwan ameongeza kuwa, kuuawa shakhsia wa kisiasa kunapasa kukomeshwa kwa sababu kitendo cha kuuwa mtu ni jinai dhidi ya ubinadamu. Ahmad bin Muhammad al Jarwan ameyataka makundi na vyama vyote vya kisiasa huko Misri kuacha kuchochea machafuko na badala yake kufanya mazungumzo na kutafuta njia ya kisiasa ili kurejesha utulivu na umoja nchini humo.
Vilevile amewaomba viongozi wa serikali ya mpito ya Misri kuunga mkono maandamano ya amani ya wananchi na kulinda haki yao ya uhuru wa kujieleza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni