Duru za habari zinaripoti kuwa, Waziri Mkuu wa zamani wa Mali,
Ibrahim Boubacar Keita anaongoza kwenye matokeo ya awali ya uchaguzi wa
rais uliofanyika Jumapili ya jana.
Habari zaidi zinasema huenda Keita akashinda uchaguzi huo katika duru ya kwanza. Maelfu ya wafuasi wake wameanza kukusanyika kwenye makao makuu ya chama cha Rally for Mali kinachoongozwa na mwanasiasa huyo. Maelfu ya wafuasi wengine pia wamekusanyika nyumbani kwa Keita mjini Bamako.
Wachambuzi wa mambo wanasema ushindani mkali unaonekana ni kati ya Ibrahim Keita mwenye umri wa miaka 69 na waziri wa zamani wa fedha, Soumaila Cisse mwenye umri wa miaka 63. Uchaguzi huo wa Mali ni wa kwanza wa kidemokrasia tangu kutokee mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa madarakani Rais Amadou Toumane Toure mwanzoni mwa mwaka uliopita.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni