KIBAKA ANUSURIKA KUFA KWA KIPIGO CHA WANANCHI KAWE
Mtuhumiwa
wa wizi akiomba kusamehewa wakati mtu mwenye hasira kali akijiandaa
kumtupia tofali kichwani ambalo lilimjeruhi vibaya mtuhumiwa huyo.
Mwananchi mwenye hasira akimsulubu mtuhumiwa huyo kwa teke.
Akisulubiwa kwa bakora na mmoja wa wananchi waliochoshwa na wizi.
...Akiendelea kusulubiwa kabla ya kupelekwa polisi.
Baada ya kulainika akawa anapelekwa polisi.
Kutokana
na kipigo jamaa huyo alianguka hatua iliyofanya watu hao wenye hasira
kutawanyika eneo la tukio, wakidhani mtuhumiwa amekufa.
MTU mmoja aliyetuhumiwa kuwa ni mwizi amenusurika kufa baada ya kundi
la wananchi kumpa kipigo cha maana, leo mchana katika eneo la
Mbezi-Darajani, Kawe mjini Dar es Salaam. Mtu huyo ambaye jina lake
halikuweza kupatikana mara moja inadaiwa alikutwa akiruka geti kuingia
ndani kwenye nyumba ya mkazi moja wa eneo hilo. Picha zifuatazo ni
baadhi ya matukio wakati mtuhumiwa huyo alipokuwa akipata kichapo hicho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni