Jumamosi, 13 Julai 2013

Marekani yataka Mursi aachiwe huru

Marekani imeitaka Misri kumuachia huru rais aliyepinduliwa, Mohamed Mursi, huku wafuasi wa kiongozi huyo wakiapa kuendeleza mapambano hadi pale atakaporejeshwa madarakani. Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Marekani, Jen Psaki, amesema nchi yake inakubaliana na rai ya Ujerumani ya kutaka Mursi aachiwe huru.
Kwa mujibu wa viongozi wa mpito wa Misri, Mursi amewekwa mahali salama, na hajaonekana hadharani tangu alipoangushwa tarehe 3 Julai.
Marekani inataka kumalizika kwa usiri juu ya mahali alipo rais huyo wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Misri, huku Ujerumani ikitaka shirika linaloaminika kimataifa kama Msalaba Mwekundu liruhusiwe kukutana na kiongozi huyo.
Jana, pande zinazopingana kuhusu suala la Mursi zilifanya maandamano mjini Cairo, ambayo yaliendeshwa kwa amani kinyume na ilivyohofiwa kuwa yangetokea makabiliano.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni