
Mawaziri walioachia ngazi ni Hisham Zaazou (Utalii), Atef Helmi (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano), Hatem Bagato (Sheria na Masuala ya Bunge) na Khaled Abdul-Aal (Mazingira). Habari zaidi zinasema mawaziri hao wamekabidhi barua zao za kujiuzulu kwa Waziri Mkuu, Hisham Qandil. Wachambuzi wengi wanakubaliana kuwa hatua hiyo ni pigo kwa serikali ya Rais Mohammad Mursi hususan wakati huu ambapo kiongozi huyo anakabiliwa na mashinikizo ya umma ya kujiuzulu.
Huku hayo yakijiri, maandamano yanaendelea katika miji mbalimbali ya Misri. Waandamanaji katika miji ya Alexandria, Suez na Port Said wamevamia na kuchoma moto ofisi za chama cha JEP cha Rais Mursi. Wapinzani wamesisitiza kwamba wataendelea na maandamano hadi pale Dkt. Mursi atakapojiuzulu.
Wakati huo huo jeshi la Misri limewapatia wanasiasa wa nchi hiyo mudaa wa masaa 48 kutatua mgogoro wa sasa wa nchi hiyo la sivyo wataingilia kati ya kuamua mustakbali wa nchi hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni