Rais wa awamu ya nne wa Kenya
Uhuru Kenyatta aliapishwa tarehe 9, Aprili, mwaka huu. Kwenye sherehe ya
kuapishwa kwake, rais Kenyatta aliahidi kuboresha haki za wanawake,
kuleta nafasi nyingi za ajira, kuendeleza uchumi wa taifa, na kutenga
fedha zaidi kwa ajili ya mambo ya elimu, matibabu na kilimo. Sasa siku
100 zimepita toka rais Kenyatta aingie madarakani. Akihojiwa na
mwandishi wetu wa habari, mhadhiri wa siasa katika Chuo Kikuu cha
Nairobi Bw. Mule Musau anaeleza kuridhishwa na kazi alizofanya rais
Kenyatta katika miezi mitatu iliyopita.
Bw. Musau anasema kutokana na hatua zilizochukuliwa na serikali yake, Kenyata anatekeleza ahadi alizotoa kwenye sherehe ya kuapishwa kwake, na hali ya uchumi wa Kenya ni tulivu na uchumi unafufuka kwa kasi. Lakini Bw. Musau amesema kutokana na hali mbaya ya uchumi wa dunia na msingi dhaifu wa uchumi wa Kenya, utekelezaji wa sera husika unakabiliwa na changamoto mbalimbali. Bw. Musau ametoa mfano wa huduma za wajawazito kujifungua bure, akisema sera hiyo bado inapaswa kurekebishwa kufuatia ukosefu wa madaktari, wauguzi na vifaa. Na mgomo wa walimu uliodumu kwa wiki nyingi mfululizo umewafanya baadhi wa wakenya waone kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya kununua kompyuta katika shule za msingi zinapaswa kutumika kuongeza mishahara ya walimu.
Vilevile, maendeleo ya uchumi wa Kenya pia yanakabiliwa na matatizo na vikwazo vingine. Watu milioni 40 nchini Kenya wanaishi katika umaskini, na karibu nusu ya Wakenya wote wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku. Hali duni ya miundo mbinu ya umeme na barabara pamoja na kukosekana kwa uwiano katika maendeleo ya mijini na vijijini pia imekwamisha maendeleo endelevu ya Kenya.
Kutokana na sababu hizo, Bw. Musau amesema Kenya inapaswa kutilia mkazo katika kuboresha utoaji wa nishati, kuhimiza marekebisho ya viwanda, kuongeza uwezo wa uzalishaji wa bidhaa, kuondokana na hali ya kutegemea kuagiza bidhaa kutoka nje, na kuendeleza biashara ndani ya nchi za Afrika. Bw. Musau anaona kuwa katika kipindi cha mtangulizi wa Kenyata Bw. Mwai Kibaki, hatua za kusamehe kodi na kutoa ruzuku kwa wawekezaji zilivutia makampuni kama Nokia, Coca Cola na IBM kuwekeza nchini Kenya, hali ambayo imehimiza mchakato wa viwanda nchini Kenya, na huenda rais Kenyata ataendelea kutekeleza mpango wa maendeleo ya uchumi ifikapo mwaka 2030 unaojulikana kama Ruwaza ya mwaka 2030 uliopendekezwa na Kibaki, na kuimarisha mawasiliano ya kibiashara na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Pamoja na kwamba Kenya bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali, Bw Musau ana matumaini na mwelekeo wa maendeleo ya Kenya katika siku za baadaye, na anaona kuwa serikali ya awamu mpya inaweza kuongoza nchi hiyo kupata maendeleo na neema. Uchambuzi mbalimbali pia umeonesha imani kwa hali ya Kenya katika siku za baadaye. Makadirio yaliyotolewa na Wizara ya Fedha ya Kenya yanaonesha kuwa mapato ya kifedha yatafikia dola za kimarekani bilioni 11.77 katika mwaka 2013/2014, hili ni ongezeko la asilimia 17.3. Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Benki ya Dunia pia inasema uchaguzi mkuu ulio amani na kugunduliwa mafuta na gesi vimeufanya uchumi wa Kenya uwe na mustakbali mzuri, na katika kipindi cha miaka mitatu ijayo ukuaji wa uchumi unatarajiwa kufikia asilimia 5 kwa mwaka.
Ingawa bado ni mapema kutabiri hali ya Kenya katika siku za baadaye kutokana na kazi zilizofanywa na serikali mpya ya Kenya katika miezi mitatu iliyopita, lakini wachambuzi wanaona kuwa kama serikali hiyo inaweza kudumisha utulivu wa kisiasa, kutekeleza bila kusita sera za uchumi za sasa, kuimarisha kihalisi uhusiano na nchi zinazoibuka kiuchumi hivi karibuni, nchi hiyo itatimiza lengo la kufufua uchumi wake na kuondokana na umasikini.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni