

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
HUDUMA YA MAWASILIANO YA VODACOM YAREJESHWA
• NI BAADA YA MOTO KUUNGUNZA MITAMBOHUDUMA YA MAWASILIANO YA VODACOM YAREJESHWA
• MTANDAO ULIZIMWA KWA SAA 16 NCHI NZIMA
Dar es Salaam, Agosti 18, 2013...
Baada ya kukosekana kwa huduma za mtandao wa Vodacom kwa takribani
masaa 16, huduma hizo zimerejeshwa katika hali yake ya kawaida asubuhi
ya Jumamosi ya Agosti 17.
Akizungumzia tatizo lililosababisha
kukosekana kwa huduma za mawasiliano kwa watumiaji wa mtandao huo,
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza amesema chanzo cha
kukatika kwa mawasiliano nchi nzima siku ya Ijumaa ni moto uliotokea
katika mtambo mkuu wa kuendeshea mtandao (Main Switch) uliyoko Dar es
Salaam.
“Kufuatia hatua hiyo, hatukuwa tena na
uwezo wa kutoa huduma kwa watu wote kuanzia siku ya Ijumaa jioni hadi
Jumamosi asubuhi, hali hii iliathiri wateja wetu wote kwa ujumla kwani
walishindwa kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki ambao wote ni wateja
wetu, alisema Meza.
Aidha aliomba radhi kwa jamii ya Watanzania
na wateja wa Mtandao wa Vodacom kwa kukosa mawasiliano katika kipindi
hicho, na kusema kuwa wateja wote wa mtandao wa Vodacom watarudishiwa
gharama zote kwa huduma yoyote walionunua na kuhitaji kuitumia wakati
ambapo mtandao haukuwa unapatikana, “Fidia hizi kwa wateja wetu wote
zitatolewa siku ya Jumatatu ya Agosti 19, 2013 alisema Meza.
“Tunaishi katika dunia ambayo mawasiliano
ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku hivyo tunaelewa kuwa tatizo
hili limekuwa kikwazo kikubwa kwa wateja wetu, Na tunawashukuru kwa kuwa
waelewa na wavumilivu katika kipindi chote ambacho tumekuwa
tukikabiliana na tatizo hili, alisema Meza.
Meza alihitimisha kwa kuhakakikishia
Watanzania na wateja wa Vodacom kwa ujumla kuwa Vodacom imedhamiria
kuendelea kutoa huduma zenye viwango vya hali ya juu nchini.
“Ninapenda uwashukuru wafanyakazi wetu wote
na washirika wetu ambao kwa pamoja wamefanya kazi bila kuchoka katika
kuhakikisha huduma zote zinarejea hadi katika hali ya kawaida hadi
kufikia Jumamosi asubuhi, Jitihada zao na kazi kubwa waliyoifanya
imewezesha huduma zote kurejea katika hali ya kawaida, alihitimisha
Meza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni