Jumamosi, 3 Agosti 2013
Juice nyingi ni feki
JUISI
Katika hali ya kawaida, juisi ni kinywaji baridi kisicho na kilevi wala
madhara kwa mnywaji. Lakini utakuwa sahihi ukizungumzia juisi
zilizotengenezwa kwa matunda halisi bila kuongezewa vitu vingine. Katika
zama hizi, hali iko tofauti, juisi nyingi tunazodhani ni vinywaji
baridi visivyo na madhara kwa afya zetu na za watoto wetu, hali haiko
hivyo.
Juisi nyingi zinazouzwa kila sehemu ni feki. Ni jambo lakusikitisha
kuona jinsi binadamu anavyojaribu kushindana na Mungu kwa kutengeneza
vitu vinavyofanana na vile alivyoumba Mwenyezi Mungu kwa ajili yetu.
Juisi nyingi hutengenezwa kwa kuchanganya maji, sukari na rangi
zilizotengenezwa kwa kemikali mbalimbali zikiwemo zenye ladha ya
matunda.
Juisi za aina hii ndiyo nyingi na zinapatikana kila kona ya nchi hii,
waathirika zaidi wakiwa watoto wetu ambao hupenda kunywa kwa kufuata
utamu wa sukari nyingi zilizowekwa na ladha za matunda.
Utafiti umeonesha kemikali (Additives) zinazowekwa kwenye vinywaji hivi,
hudhoofisha kinga ya mwili na huwa chanzo cha magonjwa ya saratani na
mengine hatarishi. Nakusihi kuacha kunywa kabisa juisi hizo na usimpe
mwanao, unamuua.
Ukiacha hizo juisi zinazotengenezwa kwa kutumia kemikali ‘mwanzo
mwisho’, kuna juisi zingine zinazodaiwa kutengezwa kutokana na matunda,
zipo za ‘machungwa’, nanasi’, ‘pasheni’, n.k. Yapo makampuni pia
yanayojitapa kutengeneza juisi zao asilimia 100 kutokana na matunda na
kwamba hakuna kinachoongezwa kingine. (100% fruit, No sugar added au No
additives, huandika hivyo kwenye maboksi yao au makopo wanayoweka juisi.
Hata hivyo, utafiti wa hivi karibuni umeonesha kuwa makampuni mengi
yanadanganya walaji.
Kwa sababu siyo kweli kwamba hawaongezi kitu kingine katika
utengenezaji wa juisi zao za matunda. Imejulikana kuwa huweka vitu vya
kufanya juisi ya kwenye boksi au chupa ikae kwa muda mrefu bila
kuharibika, halikadhalika huweka vitu vya kuifanya juisi hiyo kuwa na
ladha moja.
Acha nikupe mfano. Katika hali ya kawaida, ukichuma machungwa matano ya
mti mmoja, lazima yatakuwa na ladha tofauti, yote hayawezi kuwa na ladha
sawa japo yote yanatoka mti mmoja.
Kwa maana hiyo, kama ukitengeneza juisi kwa kutumia machungwa
yaliyochumwa kutoka miti tofauti, ladha ya juisi lazima itatofautina.
Lakini utashangaa kuona ladha ya jusi za maboksi zote zinafanana.
Wanachofanya ni kuweka ladha moja kwenye utengenezaji wa juisi zao kabla
ya kupeleka kwa mlaji. Halikadhalika, juisi ukishaitengeneza, haiwezi
kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika.
Kwa hiyo, ili kuifanya juisi hiyo iweze kukaa kwa muda mrefu bila
kuharibika, lazima iwekewe kemikali ya kuihifadhi isiharibike.Kwa
kuongezewa vitu hivyo, hata kama
Kwa maelezo hayo, hatushauriwi sana kunywa juisi hizo ‘ready made’ kwa
sababu zimekosa uhalisia, kwani zina madhara kwa afya zetu, licha ya
maelezo na matangazo mazuri tunayopewa na watengenezaji.
Badala yake tutengeneza juisi majumbani mwetu wenyewe kwa kutumia
matunda halisi ili kupata faida katika miili yetu.
Jiepushe na matumizi ya sukari nyingi katika juisi unayoitengeneza
mwenyewe, kwani kwa kufanya hivyo utakuwa unaiharibu, weka sukari kidogo
sana ikiwezekana acha kabisa.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni