
Mashabiki wa Brazil kwenye fainal ya kombe la mabara
Shirikisho la soka duninai FIFA imesema kuwa zaidi ya tiketi milioni moja za kombe la dunia zimeombwa kupitia mtandao wake ndani ya saa saba pekee tangu zianze kuuzwa.
Wengi walioagiza tiketi hizo ni mashabiki kutoka Brazil, Argentina, Marekani na Uingereza.Halmashauri ya Utalii nchini Brazil imetoa wito kwa FIFA pamoja na wamiliki wa mahoteli nchini humo kupunguza bei za juu walizoweka wakisema kuwa inaharibia jina nchi hiyo.
Bei hizo zimepanda maradufu tangu matayarisho ya kombe la Dunia yashike kasi.
Mashabiki wa soka wanaweza kuomba tiketi hizo kupitia mtandao wa FIFA hadi tarehe kumi Oktoba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni