Ni tukio la kushangaza ambalo pia limewavuta watu wengi nchini humo kwa mara ya kwanza kutokea
Tukio hilo lililoibua mshangao miongoni mwa watu walioshuhudia lilitokea katika kanisa la mtakatifu Peter mjini Nakuru.
Maharusi waliojawa na furaha isiyo na kifani walielezea kuwa malezi yao bora yaliwafanya wote kuchagua kufunga ndoa siku moja.
Samson Wachira, ambaye ni wa kwanza kuzaliwa
alisema wazazi wao waliwaonyesha kupendana na kushirikiana katika mambo
yote tangu wakiwa wadogo hali iliyowapelekea kukua katika mazingira
hayo.
Hivyo basi, Wachira alielezea kuwa kila mmoja wao alipotaka kufunga ndoa rasmi, aliwaita nduguze kwa ushauri.
Wachira ana mika 36 ilhali George Wango, ambaye ni wa mwisho kuzaliwa ana umri wa miaka 24.
Wengine walikuwa Peter Mbugua, 35, Stephen Kinyanjui, 34, na Harman Kago,32.
Ndugu hao waliitaja siku hiyo kama ya furaha
ambayo walikuwa wakiingojea kwa hamu kubwa kutokana na kufikia kupiga
hatua moja maishani mwao .
“Tumekuwa tukiingoja na kujitayarisha kwa siku hii kwa mwezi mmoja uliopita,” alisema Wango, mmoja wa maharusi hao
Wazo la kufunga ndoa siku moja liliwajia ndugu hao
miezi saba iliyopita wakati kasisi mmoja alipowatembelea nyumbani kwao
eneo la Kiratina.
Baba yao aliandaa karamu na ibada ya misa ya
shukrani wakati kasisi alitaka kujua ni nani kwa familia hiyo alikuwa
amekubaliwa kupokea sakramenti.
Kulingana na desturi za kanisa la Katoliki, ni
sharti mwanamume awe amefunga ndoa rasmi kanisani ili kuruhusiwa kupokea
sakramenti hivyo kasisi huyo aliwapa changamoto vijana hao kuhusu faida
za kufunga ndoa kanisani.
Baada ya kushauriana baina yao, vijana hao walienda kuomba
mawaidha kutoka kwa baba yao James Kago ambaye aliwapa moyo na
kuwahamasisha kufunga ndoa siku moja.
“Niliwahimiza wafunge ndoa siku moja kwani hii
ingewawezesha kufanya haraka, kupunguza gharama na zaidi ya hayo
kuwaunganisha,” alisema Kago
Kwa mwezi mzima uliopita, familia ya Kago ilikua
ikizunguka kwa wazazi wa wakwe zao watarajiwa mmoja baada ya mwingine
ili kupeleka mahari na kuomba idhini ya kufunga ndoa rasmi.
Kinyume na wengi, wanawake waliokuwa wakiolewa walimsifu sana mama mkwe hasa kwa kuunga mkono ndoa hizo na kuwashauri
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni