Rais wa Zimbabwe ayatishia makampuni ya US na UK
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametishia kulipiza kisasi kwa namna aliyoitaja kuwa ni ya “tenda nikutende” dhidi ya makampuni ya Uingereza na Marekani yanayoendesha shughuli zao huko Zimbabwe iwapo nchi za Magharibi zitaendelea kuishinikiza serikali yake kwa vikwazo na kwa kile alichokiita kuwa bughudha. Mugabe amesema kuwa Uingereza ina makampuni kadhaa huko Zimbabwe na kwamba hakuna vikwazo wala vizuizi vyovyote yaliyowekewa makampuni hayo. Amesema wakati utafika ambapo Zimbabwe itaamua kuchukua hatua za kulipiza kisasi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni