Nchini Senegal refa Mwislamu
amesimamisha mechi ya soka ili kupata fursa ya dakika chache kufuturu na
wenzake baada ya saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Ripoti zinasema kuwa mechi kati ya timu
za Casa Sport na Yeggo ilianza dakika 30 kabla ya adhana ya Magharibi na
hivyo refa Ousseynou Gueye alilazimika kusimamisha mechi hiyo kwa muda
mfupi ili aweze kufuturu.
Baada ya mechi, refa huyo alisema
anafahamu kuwa kitendo chake kinakiuka kanuni za soka lakini alichukua
uamuzi huo kwa mujibu wa mafundisho ya dini yake ya Kiislamu. Amesema
baada ya kufuturu kwa tende na maji aliweza kuendelea na kazi yake akiwa
na nishati zaidi katika mechi hiyo ya Julai 14 iliyomalizika kwa sare
bila mabao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni