Watu 24 wafariki dunia baada ya feri kuzama Uflipino
Watu wasiopungua 24 wameaga dunia na wengine zaidi ya 270
wametoweka baada ya feri ya kuvushia abria kugongana na meli ya mizigo
huko katikati mwa Ufilipino. Ajali hiyo ilitokea jana umbali wa kilomita
mbili kutoka pwani katika bandari ya Cebu katikati mwa Ufilipino. Feri
ya MV Thomas Aquinas iliyokuwa imebeba abiria 870 ilikuwa ikielekea
katika bandari ya Cebu ambapo iligongana na meli ya mizigo na
kusababisha ajali hiyo ambapo feri ilizama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni