Jumatatu, 30 Septemba 2013

Chuo kilichovamiwa Nigeria kilikosa ulinzi


mauaji ya Nigeria
Maafisa wa utawala nchini Nigeria wanasema kuwa hapakuwa na ulinzi katika chuo cha mafunzo ya kilimo nchini Nigeria ambako hadi wanafunzi 50 waliuawa Jumapili.
Wanafunzi waliuawa na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kiisilamu katika mabweni yao katika jimbo la Yobe , Kaskzini Mashariki mwa Nigeria.
Afisaa mmoja aliambia BBC kuwa serikali itashirikiana na jeshi kuhakikisha kuna ulinzi katika shule.
Serikali ya Nigeria ilisema kuwa haitafunga shule zingine kutokana na shambulio lililowaua wanafunzi 50 katika chuo kikuu cha mafunzo ya kilimo.
Shambulio hilo linashukiwa kufanywa na wanamgambo wa Boko Haram siku ya Jumapili.Wavamizi walishambulia kwa risasi chuo hicho kilichoko jimbo la Yobe, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Afisa mmoja wa serikali Abdullahi Bego, ameambia BBC kuwa serikali na idara ya jeshi zitaongeza usalama katika taasisi zote za elimu.
Eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria limewekwa katika hali ya hatari kufuatia mashambulio yanayofanywa kila mara na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram.
Boko Haram wanadaiwa kupigana kwa lengo la kuiondoa serikali iliyoko na badala yake kuweka utawala wa kiislamu. Tayari wamefanya mashambulio kadhaa katika shule.

Vyombo vya usalama

Mwandishi wa BBC wa idhaa ya Hausa, Mansur Liman, anasema kuwa huenda jeshi la Nigeria imelegeza juhudi zake kufuatia kufanikiwa kwao katika siku za hivi punde kuwaondosha wapiganaji wa Boko Haram kutoka maeneo mengi kaskazini mashariki.
Hata hivyo wapiganaji hao wameripotiwa kuiba sare za kijeshi katika siku kadhaa zilizopita na magari ya kivita. Inadaiwa wanatumia vifaa hivi kupenya maeneo yaliyowekwa ulinzi mkali.
Mshauri mkuu wa serikali katika Jimbo la Yobe, Abdillahi Bego, ameambia BBC, Jumatatu, kuwa hakukuwepo walinzi katika eneo hilo wakati shambulio lilifanywa katika chuo kikuu.
Amesema kuwa maafisa wa usalama wa Nigeria walistahili kuimarisha doria katika taasisi za elimu zote.
Amesisitiza kuwa shule zingine hazitafungwa kwani hilo ndilo hao ''magaidi'' wanataka.

Watu 39 hawajulikani walipo Nchini Kenya tangu kutokea kwa mkasa wa shambulizi la kigaidi katika Jumba la Biashara la Westgate

Jumba la Biashara la Westgate la Nchini Kenya lililoshambuliwa na Wanamgambo wa Al Shabab
Jumba la Biashara la Westgate la Nchini Kenya lililoshambuliwa na Wanamgambo wa Al Shabab
REUTERS/Thomas Mukoya

Na Nurdin Selemani Ramadhani
Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limesema idadi ya watu waliokosekana tangu kutokea kwa shambulizi la kigaidi kwenye Jumba la Biashara la Westgate Jijini Nairobi imesalia kuwa watu thelathini na tisa tofauti na hapo awali ambapo watu sitini na mmoja walikuwa hawajulikani walipo. Shirika hilo limesema idafi hiyo imepungua baada ya watu kumi na nne kupatikana wakiwa hai huku miili mingine saba ya watu waliopoteza maisha kuendelea kuwepo kwenye vyumba vya kuhifadhia maiti kitu ambacho kimechangia kushuka kwa idadi ya watu waliokuwa hawajulikani walipo.

Wakuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya wamesema hadi kufika sasa hawana taarifa za watu hao thelathini na tisa licha a kwamba usafi wa kuondoa vifusi kwenye mabaki ya jengo la Westgate kufanyika kama ambavyo Jeshi nchini humo limethibitisha.
Taarifa hii ya Shirika la Msalaba Mwekundu inatolewa huku takwimu za Serikali zikiendelea kusalia watu waliopoteza maisha kwenye shambulizi hilo wakiwa ni sabini na saba wakiwemo wanasjeshi sita ambao nao waliuawa kwenye mashambulizi na wanamgambo wa Al Shabab.
Haya yanakuja huku Mkuu wa Usalama wa Taifa nchini Kenya akiendelea kuhojiwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi akituhumiwa kushindwa kufanyia kazi taarifa za kijasusi zilizokuwepo juu ya kupangwa kwa Shambulizi la kigaidi katika Jumba la Biashara la Westgate.
Mkuu wa Usalama wa Taifa ameendelea kukabiliwa na hali ngumu ni kwa nini alishindwa kuwa na taarifa za kutosha ambazo zingesaidia kuzuia kutokea kwa shambulizi hilo la kigaidi linalotajwa kupangwa na kutekelezwa na Wanamgambo wa Kundi la Al Shabab wenye uhusiano na Mtandao wa Al Qaeda.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi nchini Kenya imefikia uamuzi huo wa kumhoji Mkuu wa Usalama wa Taifa kutokana na uwepo wa taarifa zilizovuja na kueleza Kitengo cah Usalama wa Taifa kilikuwa na taarifa za kutokea kwa shambulizi hilo tangu mwaka 2011 lakini walishindwa kuchukua hatua madhubuti kulidhibiti.
Taarifa zimeendelea kuzagaa na kuanisha Kundi la Al Shabab lilishatoa tishio la kushambulia Jumba la Biashara la Westgate pamoja na Kanisa la Mtakatifu Bsilica lililopo Jijini Nairobi lakini hakuna hatua za haraka zilizochukuliwa kuhakikisha kitisho hicho kinafanyiwa kazi kwa wakati.
Vyombo vya Habari zimekuwa vikivujisha taarifa zinazoeleza kuwa Usalama wa Taifa wa Kenya ulivyopata taarifa hizo za onyo la kufanyika kwa mashambulizi walichukua hatua za kuifahamisha Marekani na Israel ili kuhakikisha wanawasaidia kuchukua hatua kukabiliana nalo.
Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya Joseph Ole Lenku kwa upande wake amekanusha madai ya kwamba Serikali ilikuwa na taarifa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya kutokwa kwa shambulizi hilo na kusema hizo ni taarifa zisizona ukweli wowote na kama wangepata onyo hilo wangelifanyia kazi.
Lenku amewaambia wanahabari Serikali imekuwa makani katika kuhakikisha wanaimarisha hali ya usalama katika nchi yote ya Kenya kwa hiyo wanapopata taarifa kama hizo hawawezi kukaa kimya kwani wanafahamu madhara yanayoweza kutokea ni makubwa.
Katika hatua nyingine Waziri Lenku amekanusha taarifa zilizokuwa zimezagaa ya kwamba zaidi ya watu sabini wamefukiwa kwenye vifusi vilivyochangiwa na kulipuliwa kwa jengo hilo na amesisitiza hakuna mtu mwengine aliyeuawa zaidi ya wale sitini na saba waliotolea maelezo.
Kumekuwa na taarifa na hali ya wasiwasi nchini Kenya kutokana na watu kadhaa kuendelea kusaka ndugu zao ambao hawajulikani walipo huku taarifa ya mwisho ya Shirika la Msalaba Mwekundu likisisitiza watu wanaokadiriwa kufikia sitini hawajulikani walipo.
Serikali nchini Kenya imesisitiza kwenye shambulizi hilo la kigaidi la huko Westgate walifanikiwa kuwaua Wanamgambo watano waliokuwa wamewashikilia mateka na kuwaua wananchi waliokuwa kwenye Jumba hilo.

Jumamosi, 28 Septemba 2013

‘Kenya attack was rehearsed for months’

NAIROBI: The plot was hatched weeks or months ago on Somali soil, by the al-Shabaab's "external operations arm," officials say. A team of English-speaking foreign fighters was carefully selected, along with a target: Nairobi's gleaming Westgate mall.

The building's blueprints were studied, down to the ventilation ducts. The attack was rehearsed and the team dispatched, slipping undetected through Kenya's porous borders, often patrolled by underpaid — and deeply corrupt — border guards.

A day or two before the attack, powerful belt-fed machine guns were secretly stashed in a shop in the mall with the help of a colluding employee, officials say. At least one militant had even packed a change of clothes so he could slip out with fleeing civilians after the killings were done. That is the picture emerging from American security officials of the massacre at the Westgate mall, which killed scores of people over the weekend.

After a four-day standoff, President Uhuru Kenyatta of Kenya claimed on Tuesday to have finally "ashamed and defeated our attackers."

American officials said that they had not determined the identities of the attackers and were awaiting DNA tests and footage from the mall's security cameras, but that they did know the massacre had been meticulously planned to draw "maximum exposure." "They had people in there, they had stuff inside," said an American security official. "This was all ready to go when the shooters walked in."

Watu 8 bado wanashikiliwa na polisi Kenya

Polisi wa Kenya na wananchi wengine katika jengo la Westgate huko Nairobi September 21, 2013.
Polisi wa Kenya na wananchi wengine katika jengo la Westgate huko Nairobi September 21, 2013.
ukubwa wa habari
Maafisa wa Kenya wanasema bado wanawashikilia watu wanane kuhusiana na shambulizi la siku nne lililosababisha vifo kwenye jengo la maduka ya kifahari mjini Nairobi.

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Kenya, Joseph Ole Lenku aliwaambia waandishi wa habari Ijumaa kwamba maafisa wamewaachia washukiwa wengine watatu.

Mwanzoni mwa wiki hii maafisa walisema washukiwa wanamgambo watano waliuwawa wakati wanajeshi na polisi walipokuwa wakifanya operesheni ya kukomboa jengo la Westgate. Idadi rasmi ya vifo kutokana na shambulizi hilo imefikia 72.

Wachunguzi wanaendelea kupekua kwenye vifusi vya jengo hilo lililoanguka Ijumaa ya wiki iliyopita. Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya lilisema watu 59 bado hawajulikani walipo kutokana na shambulizi hilo.

Lenku alisema hakuna miili yeyote iliyopatikana kutoka kwenye eneo la tukio. “kwa mujibu wa rekodi za polisi, hakuna ripoti rasmi ya watu waliopotea ambao yawezekana walikuwa kwenye jengo hilo wakati shambulizi likitokea”.

Kundi la wanamgambo wa al-Shabab lenye makao yake nchini Somalia lilidai kuhusika kwa shambulizi na linaapa kufanya mashambulizi zaidi dhidi ya Kenya.

Katika mtandao wa Twitter Ijumaa kundi hilo la wanamgambo lilisema shambulizi lake kwenye jengo la Westgate lilikuwa ni mwanzo wa mashambulizi yanayotarajiwa kufanywa nchini humo.

Jumanne, 24 Septemba 2013

Wanajeshi 3 wa Kenya wameuawa Westgate


 
Wanajeshi watatu wa Kenya wameuawa wakati walipokuwa wakijaribu kuokoa maisha ya watu anaoshikiliwa mateka na magaidi wa al Shabab katika jumba lenye maduka la Wastgate jijini Nairobi.
Askari wengine 8 wanaripotiwa kuwa mahututi baada ya kujeruhiwa katika mapambano hayo yanayoendelea hadi sasa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) Jenerali Julius Karangi.
Duru za Kenya zinaripoti kuwa hadi sasa watu 69 wamethibitishwa kuwa wameuawa na magaidi wanaoendelea kupigana na vikosi vya jeshi la Kenya katika jengo la maduka la Westgate.
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Amina Mohammed amesema kuwa Wamarekani wawili au watatu na Mwingereza mmoja wamehusika katika shambulizi lililofanywa na magaidi dhidi ya jumba la maduka la Westgate jijini Nairobi. Balozi Amina Mohammed amesema washambuliaji hao walikuwa wakishirikiana na wenzao katika maeneo mbalimbali ya dunia kwa ajili ya kuua watu mwishoni mwa wiki mjini Nairobi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya amesisitiza kuwa shambulizi la sasa mjini Nairobi limefanyika kitaalamu.

Wanajeshi 3 wa Kenya wameuawa Westgate

 
Wanajeshi watatu wa Kenya wameuawa wakati walipokuwa wakijaribu kuokoa maisha ya watu anaoshikiliwa mateka na magaidi wa al Shabab katika jumba lenye maduka la Wastgate jijini Nairobi.
Askari wengine 8 wanaripotiwa kuwa mahututi baada ya kujeruhiwa katika mapambano hayo yanayoendelea hadi sasa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) Jenerali Julius Karangi.
Duru za Kenya zinaripoti kuwa hadi sasa watu 69 wamethibitishwa kuwa wameuawa na magaidi wanaoendelea kupigana na vikosi vya jeshi la Kenya katika jengo la maduka la Westgate.
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Amina Mohammed amesema kuwa Wamarekani wawili au watatu na Mwingereza mmoja wamehusika katika shambulizi lililofanywa na magaidi dhidi ya jumba la maduka la Westgate jijini Nairobi. Balozi Amina Mohammed amesema washambuliaji hao walikuwa wakishirikiana na wenzao katika maeneo mbalimbali ya dunia kwa ajili ya kuua watu mwishoni mwa wiki mjini Nairobi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya amesisitiza kuwa shambulizi la sasa mjini Nairobi limefanyika kitaalamu.

Wanajeshi 3 wa Kenya wameuawa Westgate


 
Wanajeshi watatu wa Kenya wameuawa wakati walipokuwa wakijaribu kuokoa maisha ya watu anaoshikiliwa mateka na magaidi wa al Shabab katika jumba lenye maduka la Wastgate jijini Nairobi.
Askari wengine 8 wanaripotiwa kuwa mahututi baada ya kujeruhiwa katika mapambano hayo yanayoendelea hadi sasa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) Jenerali Julius Karangi.
Duru za Kenya zinaripoti kuwa hadi sasa watu 69 wamethibitishwa kuwa wameuawa na magaidi wanaoendelea kupigana na vikosi vya jeshi la Kenya katika jengo la maduka la Westgate.
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Amina Mohammed amesema kuwa Wamarekani wawili au watatu na Mwingereza mmoja wamehusika katika shambulizi lililofanywa na magaidi dhidi ya jumba la maduka la Westgate jijini Nairobi. Balozi Amina Mohammed amesema washambuliaji hao walikuwa wakishirikiana na wenzao katika maeneo mbalimbali ya dunia kwa ajili ya kuua watu mwishoni mwa wiki mjini Nairobi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya amesisitiza kuwa shambulizi la sasa mjini Nairobi limefanyika kitaalamu.

Jumatatu, 23 Septemba 2013

SAKATA LA WAVULANA WALIOOTA MATITI NA JINSI JAMII ILIVYOWATENGA


VIJANA watatu wa familia moja ya  Felipe Ramirez, wamepata balaa kubwa baada ya kuota matiti yaliyosababisha kuchekwa na vijana wenzao waliokuwa wakiwaona kuwa ni mashoga.

Vijana hao kutoka katika Jamhuri ya Dominica ni  Yeuri (17 ), Gabriel (11) na  Daniu Ramírez  (12),  hata hivyo, kwa sasa wanaishi kwa amani baada ya kufanyiwa upasuaji na kuondolewa matiti hayo. 
Baba yao mzazi, Felipe Ramirez alifanya jitihada ya kuomba msaada kupitia televisheni na magazeti ili wanawe wafanyiwe upasuaji kwani walikuwa wakiishi katika mateso kwenye jamii yao.
Baada ya kuomba msaada, Mkurugenzi wa Hospitali ya  Marcelino Velez Santana nchini humo, Dokta  Pedro Antonio Delgado aliamua kuwalipia gharama za upasuaji ambao ulichukua saa mbili.
Ramirez, alisema: “Wakati wanaingizwa katika chumba cha upasuaji nilikosa raha kwa kuhofia kama watatoka salama nao waliogopa lakini baada ya kutoka, wote tumefurahi sana.”

Magaidi Nairobi wamepata mafunzo Marekani

    Mjumbe wa Congress ya Marekani, Peter King amesema magaidi waliovamia jumba la kibiashara la Westgate jijini Nairobi, Kenya wamepata mafunzo katika nchi yake. King ambaye anatoka katika chama cha upinzani cha Republicans amesema kundi hilo pia limewafunza ugaidi baadhi ya Wamarekani pamoja na Wasomali wanaoishi huko.
    Huku hayo yakijiri, Marekani imesema inajipanga kushambulia vituo kadhaa vya kundi la kigaidi la al-shabab nchini Kenya. Marekani huenda ikashambulia vituo vingine vya makundi yenye kufurutu ada barani Afrika. Hayo yamesema na kamanda wa zamani wa jeshi la Marekani, Peter Chiarelli.
    Wakati huo huo, jeshi la Kenya likishirikiana na vyombo vingine vya usalama vya nchi hiyo, limeendelea na oparesheni kali ya kujaribu kuwaokoa mateka wanaoshikiliwa na wavamizi hao katika jengo la Westgate. Wavamizi hao wanaojumuisha raia wa kigeni kutoka nchi za Magharibi na Asia na pia raia wa Somalia walivamia jumba hilo lenye maduka mengi katika mtaa wa kifahari wa Westland siku ya Jumamosi na kuuua makumi ya watu kwa kuwapiga risasi na hadi sasa bado wanawashikilia mateka watu kadhaa ambao idadi yao bado haijajulikana. Waziri wa Usalama wa Taifa nchini Kenya, Joseph Ole Lenku amewaambia waandishi wa habari kuwa, serikali imedhibiti jengo zima la Westgate na kwamba magaidi wako katika sehemu moja kwenye ghorofa ya mwisho. Ole Lenku amewataka wanahabari kuwa makini wanaporipoti tukio hilo. Habari za hivi punde zinatupasha kuwa, mmoja wa magaidi amekamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta akijaribu kuelekea uturuki. Hadi tunakwenda hewani bado oparesheni ya kujaribu kuwakamata magaidi na kuwaokoa mateka ilikuwa ikiendelea.

    Kenya yasema jitihada ya kuwaokoa mateka kumalizika hivi karibuni


    Jeshi la Kenya limethibitisha mapema leo kuwa jitihada ya kuwaokoa watu waliotekwa nyara katika shambulizi la kigaidi lililotokea jumamosi ndani ya jengo la maduka la Westgate nchini humo inakaribia kumalizika, huku idadi ya vifo ikiongezeka na kufikia 69.
    Msemaji wa jeshi la ulinzi la Kenya Kanali Cyrus Oguna amesema, jeshi hilo limefanikiwa kuwaokoa watu wengi, na kusema ni watu 10 tu bado wako ndani ya jengo hilo. Amesema askari wanne wa jeshi hilo walikimbizwa hospitali baada ya kujeruhiwa walipokuwa wakijaribu kuwaokoa watu wanaoshikiliwa ndani ya jengo hilo. Milio ya risasi imesikika mapema leo ndani ya eneo hilo ambako kundi la magaidi bado linawashikilia mateka wachache.
    Kati ya watu waliouawa katika shambulizi hilo, ni raia wawili wa Ufaransa, raia wawili wa Canada, raia watatu kutoka Uingereza, mmoja kutoka China na mmoja anatokea Ghana.
    Wakati huohuo, kufuatia shambulizi la kigaidi lililotokea mjini Nairobi, viongozi wa kimataifa wamejitokeza kwa wingi kuiunga mkono Kenya. Rais Barack Obama wa Marekani, na mawaziri wakuu kutoka Uingereza, Canada, Israel, na India, pamoja na viongozi wa kikanda kutoka nchi za Rwanda, Uganda, Tanzania, Burundi, Sudan Kusini, waziri mkuu wa Ethiopia, na nchi nyingine za Afrika wamelaani vikali shambulizi hilo, na wamesema wako tayari kutoa msaada wowote unaotakiwa na serikali ya Kenya.

    AL-SHABAAB WATANGAZA MAJINA YA WAPIGANAJI WAO WALIOKO MALL YA WESTGATE KENYA




    Al Shabaab kupitia twitter yao wametoa majina ya magaidi waliopo huko Westgate Kenya.

    Ahmed mohamed isse 22yrs from st paul minnesota
     
    Abdifath osman keenadiid 24 yrs minneapolis
     
    Gen mustafe noorudin 27 yrs kansas city
     
    Qasim said musa 22 yrs garrisa kenya
     
    Ahmed nasir shirdoon 24 yrs london
     
    Zaki jama caraale 20 yrs hargeisa somalia
     
    Ismael guled 23 yrs helsinki finland
     
    Sayid nuh 25 yrs kismayu somalia
     
    Abdirizak mouled 24 yrs ontario canada
     
    source MBONDEZ TZ

    ICC yamruhusu William Ruto kurejea Kenya


    Ruto alifikishwa ICC kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu
    Majaji katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC wameahirisha kesi ya naibu Rais wa kenya William Ruto kwa juma moja ili kumpa mda kurejea nyumbani kushughulikia hali ya kiusalama inayokumba taifa hilo.
    Watu wanoaminika kuwa magaidi wa Al Shabaab wameteka jumba la kifahari lenya maduka la Westgate jijini Nairobi na kuwazuilia mateka wakenya kadhaa.
    Bwana Ruto anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kibinadamu kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007 nchini kenya.
    Ruto na Rais Uhuru Kenyatta, wanakabiliwa na tuhuma za za uhalifu dhidi ya binadamu baada ya kudaiwa kuhusika na ghasia za kikabila baada ya uchaguzi wa mwaka 2007-2008 ambapo watu zaidi ya elfu moja waliuawa.
    Mahakama iliakhirisha kesi baada ya kikao cha dharura kuitishwa huku upande wa mashtaka ukisema kuwa hauna pingamizi lolote ikiwa kesi zitaakhirishwa kwa muda mfupi.
    Mwakilishi mmoja wa mashahidi aliangua kilio mahakamani na kutaka mahakama iweze kumruhusu Ruto kurejea nyumbani kushughulikia swala hilo la dharura.
    ''Kutokana na hali ilivyo na maoni tuliyoyasikia , mahakama inamruhusu Ruto kurejea nyumbani kwa muda wa wiki moja,'' alisema jaji anayesimamia kesi hiyo, Chile Eboe-Osuji.
    "Kwa sasa Ruto ataruhusiwa kusalia Kenya kwa wiki moja, ila ikiwa atatoa ombi lengine,'' alisema jaji Chile.
    Kwa mujibu wa wakili wa Ruto,Karim Khan, alitarajiwa kuondoka Uholanzi saa tatu asubuhi, saa za Afrika Mashariki

    Hali bado ni tete mjini Nairobi

    Makabiliano makali ya risasi na mlipuko umesikika katika jengo la Westgate mjini Nairobi, ambako jeshi la Kenya linakabiliana na baadhi ya wapiganaji wa kundi la Al shabaab wanaowazuia mateka kadhaa katika jengo hilo.
    Jumba la Westgate Jumba la Westgate
    Watu takriban 69 wameuwawa katika shambulizi hilo la Jumamosi katika eneo la maduka la Westigate huku watu wengine zaidi ya 100 wakipata majeraha mabaya. Kwa upande wake shirika la msalaba mwekundu limesema kwa sasa watu 63 hawajulikani waliko.
    Ni takriban zaidi ya saa 48 na bado polisi wanajaribu kuwaokoa mateka ndani ya jengo hilo la Westgate.
    Jeshi la Kenya likikabiliana na Al Shabaab  
    Jeshi la Kenya likikabiliana na Al Shabaab
    Polisi waliokuwa katika eneo hilo walilazimika kukimbilia mahali salama wakati palipotokea mlipuko huo.
    Jeshi la Kenya limesema kwa sasa limedhibiti ghorofa ya kwanza katika jengo hilo na wanatarajia kufanya shambulizi la mwisho dhidi ya wanamgambo hao wa Al Shabaab ambao wanaaminika kuwateka raia kwa ajili ya kujikinga na mashambulizi kutoka kwa vikosi vya usalama.
    Kulingana na mkuu wa polisi nchini Kenya, David Kimaiyo, wamefanikiwa kuwaokoa baadhi ya waliotekwa na kwa sasa wale waliobakia ndani na wanachama hao wa Al shabaab ni wachache sana.
    Magaidi hao walifika katika jengo la Westgate siku ya Jumamosi na kuanza kuwamiminia risasi raia waliokuwa katika mkahawa huo ambako watu 69 waliuwawa na wengine zaidi ya 150 kupata majeraha mabaya.
    Al Shabaab wazungumzia tukio
    Msemaji wa kundi la Al shabaab linaloaminika kuwa na mafungamano na kundi la kigaidi la Al Qaeda, Ali Mohamud Rage ameonya kwamba wale walioshikwa mateka watalipa kufuatia hatua ya jeshi la Kenya kupeleka vikosi vyake Somalia vinavyopambana na kundi hilo la Kigaidi.
    Msemaji huyo amesema iwapo Kenya inataka amani basi ni lazima iondoe jeshi lake nchini Somalia.
    Kundi la Al Shabaab Kundi la Al Shabaab
    Hata hivyo rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameapa ya kwamba kundi hilo litakabiliwa vikali na vyombo vyake vya usalama. "Tutawaadhibu wale waliotekeleza kitendo hiki na tutawaadhibu kwa nguvu zetu zote," Alisema Rais Kenyatta wakati alipokuwa anatoa hotuba yake kwa Umma hapo jana akisema kuwa mpwa wake aliyekuwa na mchumba wake waliuwawa katika shambulizi lililotekelezwa na magaidi hao wa Al Shabaab.
    Kwa sasa maafisa wa usalama nchini Kenya wanasaidiana na wenzao wa Israel pamoja na polisi kutoka Uingereza, na Marekani katika kukabiliana na wapiganaji hao. Bado miili kadhaa inaaminika kutapakaa ndani ya jengo hilo kufuatia shambulizi la siku ya jumamosi.
    Ruto arudi nyumbani kutokana na shamabulizi la Jumamosi
    Huku hayo yakiarifiwa hii leo Jumatatu mahakama ya uhalifu wa kivita ilioko The Hague Uholanzi ICC imemruhusu makamu wa rais nchini Kenya William Ruto kurudi nyumbani kwa muda wa wiki moja ili kuwa na wakenya katika wakati huu wa shambulizi.
    Makamu wa rais William Ruto Makamu wa rais William Ruto
    Ruto na mshitakiwa mwenzake mwandishi habari Joshua Arap Sang wanakabiliwa na makosa ya uhalifu dhidi ya ubinaadamu wanayodaiwa kufanya katika ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007.
    Wakati huo huo raia watatu wa Uingereza, wanawake wawili raia wa Ufaransa, watu wawili kutoka Canada akiwemo mwanadiplomasia mmoja, mwanamke mmoja raia wa China, wahindi wawili, raia mmoja wa Korea Kusini na mwanamke mmoja wa Uholanzi ni miongoni mwa waliouwawa katika shambulizi hilo.
    Hii ni kulingana na taarifa kutoka kwa serikali ya Kenya iliotangaza kuwa mjumbe wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Awoonor, aliye na umri wa miaka 78 pia aliuwawa katika shambulizi la kigaidi.

    Westgate:Mlipuko na moshi mkubwa


    Jeshi la Kenya linasema kuwa limedhibiti jengo hilo ingawa hali bado ni mbaya
    Huku hali ya mshikemshike ikiendelea kushuhudiwa katika jengo la Westgate lenye maduka, ufyatulianaji risasi umesikika ndani ya jengo hilo lenye maduka na mikahawa zaidi ya themanini.
    Milio hiyo ilidumu kwa dakika tatu na kufuatiwa na moshi mkubwa juu ya jengo hilo. Hakuna taarifa kamili kuhusu kilichosababisha moshi huo.
    Wapiganaji wa Al shabaab wamewateka nyara raia ambao idadi yao haijulikani. Walikuwemo ndani ya jengo wakiendelea na shughuli zao kuanzia Jumamosi mchana wakati wapiganaji wa Al shabaab walipowavamia na kuanza kufyatua risasi kiholela.
    Inaarifiwa kuna maiti kumi katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo.
    Aidha wapiganaji hao wanaoaminika kuwa wanachama wa Al Shabaab ni kati ya kumi na kumi na watano na bado wangali ndani ya jengo hilo.
    Ripoti zinasema kuwa ufyatulianaji mkubwa wa risasi pamoja na milipuko imesikika katika jengo hilo kwa takriban dakika 15.
    Harakati za kuendelea kumaliza operesheni hiyo zinaendelea lakini hali ya mateka walio ndani ya jengo hilo inaendelea kudorora.

    Wakenya waliofanikiwa kuondoka katika jengo la Westgate kwa usaidizi wa polisi
    Rais Kenyatta amesema kuwa jeshi linajitahidi kuhakikisha kuwa linakabiliana vilivyo na wanamgambo hao.
    Helikopta za polisi zinazunguka juu ya jengo hilo pamoja na ndege za kijeshi kushika doria. Vikosi vya usalama vinaendelea na operesheni kujaribu kuwanusuru waathiriwa wakati hali ikiwa ni ya ati ati katika eneo la shambulizi.
    Awali jeshi la Kenya lilisema limeweza kudhibiti jengo hilo lote ingawa bado limetaja hali kuwa tete mno hasa katika kujaribu kuwaokoa mateka waliosalia ndani ya jengo hilo.
    Ripoti zinasema kuwa watu 69 wamefariki katika shambulizi hilo la Al Shabaab kufikia sasa huku 175 wakijeruhiwa. Baadhi wametibiwa na kuondoka hospitalini. Baadhi ya majeraha waliyopata ni majereha ya risasi na kutokana na guruneti ambalo Al shabaab waliwarushia wale waliokuwa ndani ya mikahawa siku ya Jumamosi.
    Kundi hilo limekiri kutekeleza shambulio hilo kutokana na hatua ya Kenya kupeleka majeshi yake nchini Somalia ili kukabiliana na wapiganaji

    Matukio ya hivi punde Westgate

     
    Vikosi vya usalama vinaendelea na juhudi za kukabiliana na magaidi walioteka nyara baadhi ya wakenya katika jengo la Westgate
    Katika ukurasa huu tutakupasha moja kwa moja matukio yanavyojiri katika jengo la Westgate.
    Ikiwa uko karibu na jengo hilo unaweza kutupasha hali unavyoiona kupitia kwa ukurasa wetu wa Bofya facebook bbcswahili

    15:33 Waziri wa usalama wa Kenya Joseph Ole Lenku asema kuwa wanajeshi wameweza kudhibiti jengo lote la Westgate
    15:20 Polisi waonekana wakikimbia huku na kule katika harakati zao hizo dhidi ya Al Shabaab
    Juhudi za uokozi Westgate
    14:56 Mkuu wa majeshi Meja Jenerali Julius Karangi amesema magaidi hao wanaweza kujisalimisha ikiwa wanataka kwa sababu jeshi litakabiliana nao vilivyo. Pia amesema kuwa Kenya inakabiliana na magaidi wa kimataifa

    14:35 Ole Lenku anasema kuwa hali ingali tete lakini vikosi vya usalama vya Kenya vinakaribia kuwazingira magaidi hao...Hadi kufika sasa watu 62 wamefariki na wengine zaidi ya 175 kujeruhiwa. Pia ameongeza kuwa magaiodi wote ni wanaume, kutokana na taarifa za awali kuwa magaidi hao walikuwa wanaongozwa na mwanamke

    14:30 Ole Lenku anasema kuwa wanajeshi kumi wamejeruhiwa na wanapokea matibabu. Pia mateka karibu wote wameweza kuokolewa. Ole Lenku pia amesema kuwa wameweza kuwaua magaidi wawili

    14:28 Waziri wa usalama Joseph Ole Lenku anasema kuwa moshi ulitokana na moto uliosababishwa na magaidi wlaioko ndani ya jengo hilo kujaribu kusambaratisha juhudi za wanajeshi wa Kenya dhidi yao

    Moshi mkubwa ukitoka ndani ya jumba la Westgate
    14:03 Mkuu wa polisi David Kimaiyo asema kuwa vikosi vya usalama vinakaribia kudhibiti jengo hilo lote na vimeingia ndani kabisa ya jengo hilo kiasi cha kuwaokoa baadhi ya mateka
    14:00 PM: Milipuko zaidi yasikika katika jengo hilo

    13:54: Mwandishi wa BBCIdriss Situmaaliye katika eneo la Westgate anasema duru zinaarifu kuwa vikosi vya usalama vya Kenya vinasema kuwa ndivyo vimelipua sehemu ya jengo kujaribu kuingia ndani kabisa ya jengo hilo
    13:52 PM Magari ya Ambulance yaobnekana yakienda katika eneo la shambulizi pamoja na magari ya zima moto. Vikosi vya usalama vinawataka watu kuondoka karibu na eneo la operesheni hiyo ili kuwawezesha kufanya kazi yao

    Waathiriwa wa shambulizi la Westgate
    13:49 pm: Moshi mkubwa mweusi waonekana ukitoka juu ka juu katika jengo hilo haijulikani nini kilichosababisha
    13:19 pm Moshi mkubwa unaonekana ukitoka katika jengo la Westgate ambako wapiganaji wa Al Shabaab wanawazuilia mateka wakenya ambao idadi yao haijulikani

    13:12 PM Viongozi wa kidini watoa taarifa kulaana kitendo cha Al Shabaab
    12:30 PM: Milipuko zaidi na milio ya risasi imesikika katika jengo la Westgate huku vikosi vya usalama vikifanya jitahada za misho kuwa

    Jumapili, 22 Septemba 2013

    Manchester City vs Manchester United Highlights 4 - 1

    Manchester City vs Manchester United Highlights 4 - 1

    Changamoto baada ya uchaguzi wa Ujerumani

     Wajerumani wanasubiri kujuwa nani atakayewaongoza .Yeyote atakayeibuka mshindi baada ya uchaguzi mkuu wa leo (22.09.2013) atakabiliwa na changamoto nzito katika kipindi chake cha utawala miaka minne ijayo

    Yeyote atakaeshinda uchaguzi wa Septemba 22, anasubiriwa na mtihani mkubwa Yeyote atakaeshinda uchaguzi wa Septemba 22, anasubiriwa na mtihani mkubwa

    Uchaguzi hutanguliwa na kampeni ya uchaguzi wenyewe na wakati huo siasa hutawala. Lakini hakuna kubwa linalofanyika kwani maamuzi muhimu hubakia miezi kadhaa bila ya kutelezwa. Ukweli huu pia uko kwenye masuala muhimu katika sera ya mambo ya nchi za nje ambapo mnamo majuma machache yaliyopita, hali ilikuwa kimya. Serikali itakayokuwa madarakani baada ya uchaguzi huu mkuu itakabiliwa na changamoto kwa miaka miaka minne ijayo.
    Je mgogoro wa sarafu ya euro umefikia wapi?
    Bila shaka kitu kimoja ni wazi: Msukosuko wa euro umetulia kidogo tu, huenda ukagonga tena vichwa vya habari karibuni baada ya uchaguzi. Ingawa baadhi ya nchi za Ulaya zinafanya vizuri baada ya msukosuko huo, lakini Ugiriki haiwezi kujikwamua peke yake kwani deni lake la euro bilioni 300 ni kubwa mno.
    Angela Merkel wa CDU ambaye anapewa nafasi kubwa ya kuchaguliwa tena  
    Angela Merkel ana nafasi kubwa ya kuchaguliwa tena
     
    Hata waziri wa fedha wa Ujerumani, Wolfgang Schäuble, kutoka chama cha Christian Democratic Union,CDU, ameuambia umma kupitia bunge, Bundestag, kwamba patalazimika paweko mpango mwengine tena wa kuisaidia Ugiriki.
    Taasisi maarufu za utafiti wa masuala ya uchumi zinatarajia kwamba mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya yatakutana mwishoni mwa mwaka kuamua juu ya msaada mpya, ukiwa ni mzigo mkubwa kwa serikali mpya ya Shirikisho nchini Ujerumani.
    Deni la Bajeti ya Ujerumani: Kuweka akiba au afadhali kuamua kutoa zawadi?
    Ujerumani kwa hakika iko katika hali bora kuliko nchi nyingi nyingine za Ulaya, uchumi unakuwa na mapato ya kodi ya juu kuliko ilivyowahi kuwa. Pamoja na hayo, serikali ya Ujerumani ina deni la euro trilioni 2.1 na deni linaongezeka kila mwaka kuliko pato lake. Mikoa kadhaa ina mzigo mkubwa wa madeni na serikali nyingi za miji na mitaa ni muflisi. Takriban kila chama kinataka kuibadili hali hiyo .
      Mgombea wa chama cha SPD Peer Steinbrück. Wafuasi wake bado wanayo imani
     
    Vipi kuibadili hali hiyo: kuweka akiba zaidi au kuongeza kodi? Chama cha Social Democratic, SPD, na chama cha Kijani, alau vimetangaza vinataka wenye pato kubwa walipe kodi ya juu, hilo halikubaliwi na vyama vya CDU na FDP. Angela Merkel alisema wakati wa mjadala wa televisheni dhidi ya mpinzani wake Peer Steinbruck "Mipango ya kuongeza kodi ya Social Democratic na Kijani (Grüne) itazorotesha hali bora ilioko hivi sasa."
    Wakati huo huo, vyama vingi vinataka kutumia fedha nyingi kwa miradi wanayoipendelea. Kwa mfano CDU inataka malipo ya juu ya uzeeni kwa akina mama, SPD na Kijani, matumizi zaidi kwa elimu na huduma za watoto. Kwa hiyo Ujerumani italazimika kuwa na mpaka katika ongezeko la deni lake na hadi 2020 lazima iyaweke mambo sawa.
    Haki zaidi lakini vipi?
    Suala la haki litachukua nafasi kubwa baada ya uchaguzi. Hapa kuna mambo kadhaa. Usoni kabisa ni usawa katika elimu: Kila mtoto anapaswa kuwa na nafasi sawa katika maisha. Kwa wakati huu sivyo ilivyo nchini Ujerumani. Mtoto anayetoka familia ya wasomi na nafasi kubwa zaidi ya kupata elimu na kumaliza kidato cha sita kuliko anayetoka familia ya wasiosoma. Pia suala la usawa wa malipo katika ajira liko usoni katika orodha. “Kuna wengi wanaofanya kazi siku nzima lakini kwa malipo madogo kiasi ya hata kushindwa kukidhi mahitaji yao,” amesema mgombea ukansela wa chama cha SPD, Steinbruck. Kwa hiyo swali ni je, panapaswa kuweko mshahara wa wastani kwa wote nchini Ujerumani?

    Idadi ya watu waliouawa Kenya yafikia 59 na majeruhi 175

    Maafisa wa usalama wakizingira jengo la Westgate jijini Nairobi
    Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Kenya Joseph Ole Lenku amesema idadi rasmi ya watu waliopoteza maisha imefikia 59 wakati majeruhi 175 wakitawanywa katika hospitali mbalimbali jijini Nairobi kupatiwa msaada wa kiafya.Aidha Ole Lenku ameeleza kuwa wanausalama bado wanazingira jengo la Westgate kuhakikisha watu waliotekwa na wapiganaji wa Alshabab wanaokolewa salama na watuhumiwa hao wanatiwa nguvuni.
    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametoa pole kwa jamaa waliopoteza ngudu zao katika tukio hilo na kuwataka raia wa Kenya kushikamana na kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa wanausalama kukabiliana na tatizo hilo.
    Wanamgambo hao wa kundi la kigaidi la Al Shabab wamesema walitekeleza shambulizi hilo kwa sababu serikali ya Kenya imekataa kuyaondoa majeshi yake nchini Somalia.
    Tayari watu wengine wanne wametajwa na vyombo vya habari nchini humo kuokolewa kutoka ndani ya jengo hilo la biashara ambapo walishuhudia kuwa waliwaona watu waliokuwa wamejifunika nyuso zao wakianza kumshambulia mtu yeyote waliyekutana naye ndani ya jengo hilo jumamosi mchana.
    Inadaiwa kuwa washambulizi hao walikuwa wanamuuliza waliyekutana naye maswali ya Kislamu na yeyote aliyeshindwa kutoa jibu au kuthibitisha kuwa ni Mwislamu alipigwa risasi.
    Rais Kenyatta ametaja shambulizi hilo la kigaidi kuwa ni kitendo ambacho hakikubaliki kamwe na waliohusika watakumbana na mkono wa sheria.
    Aidha, Kenyatta amesisitiza kuwa wakenya hawatagawanyika kutokana na shambulizi hilo na jeshi lake litaendelea kukabiliana na magaidi nje na ndani ya taifa hilo.
    Makundi mbalimbali nchini humo yamejitokeza kulaani shambulio hilo na kutoa pole kwa wahanga,akiwemo waziri mkuu wa zamani Raila Odinga ambaye ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia kati mapambano hayo yanayoendelea nchini humo.
    Waziri wa Mambo ya nje wa Ungereza William Hague amesema kuwa serikali yake inashirikiana na Kenya kuhakikisha kuwa inakabiliana na suala la ugaidi na wanamgambo hao wanapatikana.
    Miongoni mwa raia wa kigeni waliopoteza maisha yao katika shambulizi hilo ni pamoja na raia wawili wa Ufaransa na Canada.
    Hili ndilo shambulizi baya zaidi kuwahi kuikumba Kenya tangu shambulizi la bomu lililotokea mwaka 1998 lilotekelezwa na Al-Qeada.

    Jumamosi, 21 Septemba 2013

    AL-SHABAB WAKILI KUSHAMBULIA WESTGATE NAIROBI.

    Al shabaab: ''Kenya ilipuuza onyo letu''


    Duka la kifahari lililoshambuliwa la Westgate katika mtaa wa Westlands Nairobi
    Afisaa mmoja mkuu wa kundi la kigaidi la Alshabaab, amefahamisha BBC kuwa kundi hilo ndilo limehusika na shambulizi dhidi ya duka la kifahari la Westage mjini Nairobi Kenya.
    Kwa mujibu wa Afisaa huyo mashambulizi hayo yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa Kenya kwa kujihusisha na vita vya Somalia ambako wanajeshi wake wanakabiliana na kundi hilo.
    Wanajeshi wa Kenya wamekuwa nchini humo tangu mwaka 2011 kama sehemu ya juhudi za muungano wa Afrika kutaka kurejesha uthabiti nchini Somalia.
    Afisaa mkuu wa mambo ya ndani Kenya amesema idadi ya waliofariki ni kumi na moja lakini shirika la msalaba mwekundu linasema idadi hiyo imefika watu 30 huku zaidi ya hamsini wakijeruhiwa.
    Taarifa kutoka Ikulu ya Rais Kenya zinasema kuwa mshukiwa mmoja aliyekamatwa alifariki kutokana na majeraha yake.
    Baadhi ya watu waliofanikiwa kukimbilia usalama wao
    Wanamgambo wa Al Shabaab kupitia kwa mtandao wao wa Twitter , wanasema kuwa Kenya haikuchukulia kwa uzito onyo walilotoa kwa taifa hilo kwa hatua ya kuwapeleka wanajeshi wake nchini humo kupambana dhidi yao.
    Kundi hilo limesema limekuwa likitoa onyo mara kwa mara kwa Kenya kuwa ikiwa haitaondoa vikosi vyake nchini Somalia, athari zitakuwa mbaya mno.
    Kupitia mtandao wao wa Twitter, Al Shabaab limesema kuwa Kenya ilijidai kutosikia onyo hizo, na kuendelea kuwaua waisilamu wasio na hatia nchini Somalia.
    Taarifa hiyo ya Twitter ilisema kuwa Shambulio la Westgate ni tone tu katika bahari ya mfano wa yanayowakumba wasomali nchini Somalia.
    Taharuki ilianza hii leo saa saba mchana wakati watu wanaokisiwa kuwa kumi walipovamia jengo la kifahari la Westgate la kuwapiga risasi kiholela wakenya waliokuwa wanaendelea na shughuli zao za kawaida.
    Kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu , takriban watu 30 walifariki kwa kupigwa risasi au kutokana na majeraha yao na wengine wengi wenye majeraha ya risasi kukimbizwa hospitalini kwa matibabu

    CHELSEA VS FULHAM -2-0

                                    TAZAMA HIGHLIGHT YA MECHI KATI YA CHELSEA NA FULHAM 2-0

    Dr. Slaa kuunguruma Washington D.C., Sept. 22, 2013


    ----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

    Saturday, September 14, 2013

    Dr. Slaa kuunguruma Washington D.C., Sept. 22, 2013



    Mkutano na Dr. Willibrod Slaa Jijini Washington D.C.

    Viongozi na wanachama wa CHADEMA DMV wanapenda kuwakaribisha Watanzania wote Kuhudhuria mkutano na Dr. Willibrod Slaa utakaofanyika Siku ya Jumapili September 22, 2013 Mida ya 1:pm Mchana hadi 6:pm

    Adress: 1401 Unirvesty Blvd. Langley Park. Md 20783 (Mirage Hall)
    Karibuni tuje tujadiliane kuhusu maendeleo ya nchi yetu.

    Maelezo zaidi wasiliana na Liberatus Mwang'ombe "Libe"  (240) 423-3331 Baby Mgaza (202) 200-5031,
    Hussein Kauzela (614) 653 - 1137

     waTanzania wote mnakaribishwa

    Dr. Slaa kuunguruma Washington D.C., Sept. 22, 2013


    ----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

    Saturday, September 14, 2013

    Dr. Slaa kuunguruma Washington D.C., Sept. 22, 2013



    Mkutano na Dr. Willibrod Slaa Jijini Washington D.C.

    Viongozi na wanachama wa CHADEMA DMV wanapenda kuwakaribisha Watanzania wote Kuhudhuria mkutano na Dr. Willibrod Slaa utakaofanyika Siku ya Jumapili September 22, 2013 Mida ya 1:pm Mchana hadi 6:pm

    Adress: 1401 Unirvesty Blvd. Langley Park. Md 20783 (Mirage Hall)
    Karibuni tuje tujadiliane kuhusu maendeleo ya nchi yetu.

    Maelezo zaidi wasiliana na Liberatus Mwang'ombe "Libe"  (240) 423-3331 Baby Mgaza (202) 200-5031,
    Hussein Kauzela (614) 653 - 1137

     waTanzania wote mnakaribishwa