Jumapili, 13 Oktoba 2013

Cote d'Ivoire yaichakaza Senegal 3-1, yabisha hodi kombe la dunia 2014

Washambuliaji wa Cote d'Ivoire Didier Drogba, Salomon Kalou na Gervinho
Washambuliaji wa Cote d'Ivoire Didier Drogba, Salomon Kalou na Gervinho
sportlifeworld.com

Timu ya taifa ya Cote D'Ivoire imeichakaza Senegal kwa mabao 3-1 na kubisha hodi kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014.

Washambuliaji Didier Drogba, Salomon Kalou na Gervinho wote kwa pamoja wameng'ara katika mchezo huo hapo jana mjini Abidjan, baada ya kuifungia timu yao magoli hayo matatu na kuongeza matumaini ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwakani.
Drogba alifunga kwa penalti dakika ya tano, kabla ya winga wa zamani wa Arsenal, Gervinho kufunga bao la pili dakika ya tisa na baadaye kipindi cha pili Salomon Kalou akafunga bao la tatu.
Ushindi huo unapfanya Cote d'Ivoire kuhitaji sare au kufungwa si zaidi ya wastani wa bao moja katika mchezo wa marudiano ili kujikatia tiketi ya Brazil mwakani.
Senegal yenyewe itahitaji kushinda 2-0 tu nyumbani, ili kujihakikishia kurejea Fainali za Kombe la Dunia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni