Ijumaa, 25 Oktoba 2013

Maalim Seif: Nitaendelea kugombea urais Zanzibar


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, ametangaza azma yake ya kuendelea kugombea urais visiwani humo pamoja na ukatibu mkuu wa Chama chake cha Wananchi (CUF). Akizungumza wakati wa kutathmini miaka mitatu ya utendaji wa serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar hapo jana, Maalim Seif Sharif Hamad alisitiza kuwa, atastaafu siasa pale atakapoishiwa na nguvu mwilini, na kwamba licha ya watu fulani kumuona kuwa ni kizingiti kwa matakwa yao, hataacha nia yake hiyo ya kuwatumikia Wazanzibari. Kuhusu kugombea tena nafasi yake ya ukatibu mkuu katika uchaguzi wa CUF utakaofanyika mwakani na urais wa Zanzibar mwaka 2015, Seif alisema kuwa atatoka tu endapo wanachama wataamua kutomchagua tena. Maalim Seif alianza kugombea urais wa Zanzibar kwa mara ya kwanza mwaka 1995 baada mfumo wa vyama vya vingi kurejeshwa rasmi nchini Tanzania lakini ukitoa uchaguzi uliopita, mara zote amekuwa akilalamika kwamba anapokwa ushindi na akitangazwa mgombea wa chama tawala cha CCM kuwa mshind

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni