Jumamosi, 19 Oktoba 2013

Mlipuko wa bomu waua watu 13 katikati mwa Somalia


Watu wasiopungua 13 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya kutokea mlipuko mkubwa wa bomu nje ya hoteli moja katikati mwa Somalia. Duru za usalama za Somalia zinaarifu kwamba, mlipuko huo wa bomu umetokea leo nje ya hoteli moja katika mji wa Baladweyne ulioko katikati mwa nchi hiyo. Aghalabu ya waliouawa katika mlipuko huo ni wanajeshi. Hoteli hiyo iko jirani na kambi ya jeshi mjini Baladweyne na inatumiwa zaidi na wanajeshi wa Ethiopia na wa serikali ya mpito ya Somalia. Licha ya kuwa hadi sasa hakuna kundi lililotangaza kuhusika na mlipuko huo, lakini vyombo vya usalama vya Somalia vinaliekezea kidole cha tuhuma kundi la wanamgambo wa Al-Shabab ambao wamekuwa wakiendesha mapambano dhidi ya vikosi vya serikali na majeshi ya nchi za Afrika yanayoshirikiana nayo. Hivi karibuni Umoja wa Afrika ulitangaza kuwa, unapanga mikakati ya kuongeza idadi ya askari wa kulinda amani nchini Somalia AMISOM, kwa shabaha ya kupambana na wanamgambo wa kundi la al Shabab.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni