China italegeza sheria yake inayoruhusu wanandoa kuwa na mtoto
mmoja tu kama sera ya upangaji uzazi katika taifa hilo lenye idadi
kubwa ya watu ulimwenguni na pia itafutilia mbali sheria yake ya
kuwapeleka katika kambi za mateso watuhumiwa wa makosa
madogo madogo kama hatua ya kurekebishwa tabia. Hayo
yametangazwa leo baada ya viongozi wa chama tawala cha
kikomunisti kukutana. Kubadilishwa kwa sera ya kupanga uzazi sasa
itaziruhusu familia kuwa na watoto wawili lakini iwapo tu mmoja wa
wazazi hao ni mtoto wa pekee kwao. Sera hiyo ya kuwa na mtoto
mmoja ilianzishwa katika miaka ya sabini kudhibiti idadi ya watu
katika taifa hilo lakini imekuwa ikishutumiwa na mashirika ya kutetea
haki za binaadamu kuwa inatekelezwa wakati mwingine kwa njia za
kinyama kama kulazimishwa kuavya mimba au kufungwa kizazi.
Shirika la habari la serikali, Xinhua, limesema sera hiyo itatekelezwa
hatua kwa hatua.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni