Hii ndiyo kazi ya CC-CHADEMA kwa wale wenye kutoa matamko bila kuijua katiba .
Nimewiwa kuongezea hapa na huu mchango wa kamanda Lissu.
Ibara ya 5.4.3 inasema mwanachama wa CHADEMA anaweza kuachishwa au
kufukuzwa uanachama kwa kuwa na mwenendo usioendana na itikadi,
falsafa, madhumuni na maadili ya chama. Ibara ya 5.4.4 inaeleza kwamba
Kamati Kuu inaweza kumwachisha au kumfukuza mwanachama yeyote kwa
utaratibu uliowekwa na Kanuni za Chama. Kanuni za Chama ni pamoja na
Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama, Kanuni za Kusimamia Shughuli,
Mwenendo na Maadili ya Wabunge wa CHADEMA na Mwongozo wa Kutangaza
Kusudio la Kuwania Uongozi wa Chama, Mabaraza na Serikali.
Utaratibu wa hatua za kinidhamu uko kwenye kanuni ya 6.5.2 ikisomwa
pamoja na kanuni ya 6.5.6 na 6.5.7 ya Kanuni za Uendeshaji Kazi za
Chama. Kwa kifupi, mtuhumiwa anatakiwa kupatiwa mashtaka ya maandishi
na kuambiwa ajitetee kwa maandishi sio pungufu ya wiki mbili na baada
ya hapo ana haki ya kujitetea mbele ya kikao husika cha nidhamu. Hata
hivyo, Kamati Kuu ya chama inaweza - kwa mujibu wa kanuni ya 6.5.2(d)
- kuchukua hatua stahiki za kinidhamu bila kujadili matakwa ya kanuni
zilizotajwa mwanzoni, endapo itaona kuna dharura na maslahi ya chama
yanaweza kuathirika kama hatua hizo hazijachukuliwa.
Nawaombeni msome kanuni ya 10 ya Kanuni za Uendeshaji inayohusu
maadili ya viongozi na wanachama; kanuni za 2(b), 3(b) na (f) za
Kanuni za Mwenendo na Maadili ya Wabunge; na kanuni za 2(d), (e) na
(g) za Mwongozo wa Kutangaza Kusudio la Kuwania Uongozi wa Chama.
Mkakati wa Mabadiliko 2013 unapaswa kuangaliwa kwa macho ya vifungu
vyote hivi vya Katiba na Kanuni za Chama ili kuweza kuelewa the
thinking behind uamuzi wa Kamati Kuu. Kama masharti yote yaliyoko
kwenye vifungu hivi vya sheria za Chama hayakustahili kuheshimiwa basi
Kamati Kuu itakuwa imekosea sana katika maamuzi yake. Kama masharti
haya yalistahili kuheshimiwa then kosa la Kamati Kuu ni lipi hasa?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni