Ijumaa, 6 Desemba 2013


Mandela kuzikwa jumapili 15 Desemba

Nelson Mandela (1998)
Nelson Mandela (1998)
RFI

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema kuwa Hayati Nelson Mandela atazikwa tarehe kumi na tano Jumapili mwezi Disemba katika kijiji cha Qunu mkoa wa Eastern Cape.

Rais wa Marekani Barack Obama na mke wake Michelle wataungana na raia wa Afrika Kusini juma lijayo kutoa heshima za mwisho kwa hayati Nelson Mandela wakiambatana na raisi wa zamani wa marekani George Bush na mkewe Laura Bush.
Bwana Bush ambaye alikuwepo madarakani nchini Marekani wakati Mandela akiingia madarakani huko Afrika kusini amesema ataambatana na familia yake kwenda kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi wa zamani wa afrika ya kusini.
Wananchi wamejitokeza katika sehemu nyingi za Afrika Kusini na mataifa mbalimbali wakiendelea kutuma salamu za rambirambi na kuomboleza kifo cha Nelson Mandela.
Wachambuzi wa siasa wanaona kuwa itachukua muda mrefu kwa bara kumpata kiongozi shupavu na mzalendo kama Mandela.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni