Ijumaa, 6 Desemba 2013

Matukio makubwa ya nelson mandela


na mwandishi wetu: mussa shimba

mwaka
tarehe
tukio
1918
Julai 18
Rolihlahla Mandela alizaliwa huko Mvezo, Transkei
1925

Alipata elimu ya msingi huko Ounu na kupewa jina la Nelson na mwalimu wake
1927

Alilelewa na Chifu wa Thembu Jongintaba Dalindyebo
1934

Aliendelea na masomo katika shule ya bweni ya Clarkebury huko Engcobo
1937

Aliingia Chuo cha Wesleyan cha Healdtown huko Fort Beaufort
1939

Alijiunga na Chuo Kikuu cha Fort Hare huko Alice
1940

Alifukuzuwa kutoka chuo kikuu
1941

Alikimbia ndoa iliyopangwa na wanafamilia wake, akawa mlinzi wa mgodi, na kuandika makala kwa shirika la wanasheria la Witkin, Sidelsky & Eidelman
1942

Alipata shahada ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Afrika Kusini
1942

Alianza kuhudhuria mikutano ya Chama cha ANC kama mwananchi wa kawaida
1943

Alihitimu Chuo Kikuu cha Fort Hare, na kuanza kusomea shahada ya kwanza ya sheria katika Chuo Kikuu cha Wits.
1944

Alianzisha Umoja wa Vijana wa ANC ANCYL, na kumwoa Evelyn Ntoko Mase, wana watoto wanne Thembekile (1945); Makaziwe (1947 – who dies after nine months); Makgatho (1950); Makaziwe (1954)
1948

Alichaguliwa kuwa katibu wa taifa wa ANCYL
1951

Alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa ANCYL
1952

Kampeni ya mapambano ilianza. Alichakuliwa kuwa makamu mwenyekiti wa kwanza wa ANC huko Transvaal. Baadaye alichaguliwa kuwa naibu mkuu wa ANC. Alihukumiwa kifungo cha miezi tisa jela na kazi ngumu, pamoja na Walter Sisulu, J. S. Moroka, na watu wengine 17; Afungua ofisi ya kwanza ya wanasheria weusi pamoja na Oliver Tambo
1953

Alitunga mpango mkubwa wa operesheni za kisirisiri za ANC
1955

Alishuhudia kupitishwa kwa Hati ya Uhuru
1956

Mandela na wengine 155 walikamatwa kwa tuhuma za uasi na kuachiliwa Machi 1961
1958

Aliachana na Evelyn Mase, kumwoa Nomzamo Winnie Madikizela, wana watoto wawili Zenani (1959) and Zindzi (1960)
1960
Machi 21
Mauaji makubwa ya Sharpeville

Machi 30
Hali ya hatari ilitangazwa, na Mandela ni miongoni mwa maelfu waliokamatwa

Aprili 8
ANC kilipigwa marufuku
1961

Aingia mafichoni; Kundi la Umkhonto weSizwe (MK) liliundwa
1962
Januari 11
Alikwenda nchi ya nje kupata mafunzo ya kijeshi na kutafuta kuungwa mkono kwa chama cha ANC

Agosti 5
Alikamatwa karibu na Howick, KwaZulu-Natal

Novemba 7
Alihukumiwa kifungo cha miaka mitano kwa uhalifu wa uchochezi na kwenda nje ya nchi bila pasipoti
1963
Mei 27
Alipelekwa kwenye kisiwa cha Robben

Juni 12
Alirudishwa kwenye gereza la Pretoria

Oktoba 9
Alipelekwa mahakamani kwa mara ya kwanza katika kile kilichokuja jufahamika kama kesi ya Rivonia

Disemba 3
Akana tuhuma za hujuma katika kesi ya Rivonia
1964
Juni 11
Watu wote isipokuwa Rusty Bernstein na James Kantor walihukumiwa kifungo cha maisha  jela
1969
Julai 13
Mtoto wake Thembekile alifariki katika ajali ya barabarani
1982
Machi 31
Mandela, Sisulu, Raymond Mhlaba, na Andrew Mlangeni wapelekwa gereza la Pollsmoor
1985

Alikataa pendekezo la rais PW Botha la kumwachia huru kwa sharti la kuacha vitendo vya kimabavu
1985
Novemba 3
Afanyiwa upasuaji wa kibofu cha mkojo
1988
Agosti 12
Alazwa kwenye hospitali ya Tygerberg na kugunduliwa kuwa na kifua kikuu

Agosti 31
Alazwa kwenye zahanati ya Constantiaberg

Desemba 7
Ahamishiwa kwenye gereza la Victor Verster huko Paarl ambako alishikiliwa kwa miezi 14 katika nyumba ndogo
1990
Feburari 2
Marufuku dhidi ya ANC yaliondolewa
1990
Feburari 11
Aliachiwa huru

Machi 2
Alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa ANC
1993
Desemba 10
Mandela na FW de Klerk walipewa tuzo ya amani ya Nobel
1994
Aprili 27
Alipiga kura kwa mara ya kwanza maishani mwake

Mei 9
Bunge la Afrika Kusini llilimchagua kuwa rais wa kwanza baada ya Afrika Kusini kuwa nchi ya demokrasia

Mei 10
Kuapishwa kuwa rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini

Desemba 14
Alizindua kitabu kuhusu maisha yake cha Long Walk to Freedom
1995

Alianzisha mfuko wa watoto wa Nelson Mandela
1996

Aliachana na Winnie Mandela
1998
Julai 18
Alimwoa Graça Machel katika siku yake ya kuzaliwa alipotimiza miaka 80
1999

Alistaafu baada ya kuwa madarakani kwa kipindi kimoja, na kuanzisha mfuko wa Nelson Mandela
2001

Agunduliwa kuwa na saratani ya tezi kibofu
2003

Alianzisha mfuko wa Mandela Rhodes
2004
Juni 1
Alitangaza kuwa atastaafu maisha ya hadhara
2005
Januari 6
Alitangaza kuwa mtoto wake mkubwa Makgatho alifariki kutokana na Ukimwi
2007

Alishuhudia kusimikwa kwa mjukuu wake Mandla kama chifu wa baraza la kikabila la Mvezo
2008
Julai 18
Atimiza miaka 90. Atoa wito kwa kizazi kijacho kuendelea kupigania haki za kijamii
2009

Alipiga kura kwa mara ya nne maishani mwake. Alihudhuria hafla ya kuapishwa kwa rais Jacob Zuma tarehe 9 Mei
2010

Apokea kombe la dunia la FIFA kabla halijatembezwa Afrika Kusini
2010
Juni 11
Kitukuu wake wa kike Zenani auawa katika ajali ya gari
2010
Juni 17
Ahudhuria mazishi ya kitukuu wake
2010
Julai 11
Alihudhuria fainali ya mashindano ya soka ya Kombe la Dunia huko Soweto
2010
Julai
Asherehekea miaka 92 ya kuzaliwa mjini Johannesburg akiwa na familia na marafiki
2010
Oktoba
Kitabu chake cha pili Conversations with Myself  kilianza kuuzwa
2010
Novemba 18
Akutana na timu za mpira wa miguu za Afrika Kusini na MArekani zilizoshiriki mechi ya kombe ya Mandela
2011
Januari
Alazwa hospitali mjini Johannesburg ambako anagunduliwa kuwa na maambukizi kwenye kifua. Atoka hospitali baada ya siku mbili.
2011
Mei 16
Apiga kura kwenye uchaguzi mdogo
2011
Juni
Kitabu chake cha Nelson Mandela By Himself: The Authorised Book of Quotations kilianza kuuzwa
2011
Juni 21
Alitembelewa na Michell Obama, mke wa rais wa Marekani, na watoto wake wawili
2011
Julai 18
Asherehekea miaka 93 ya kuzaliwa na familia yake huko Qunu, Eastern Cape
2011
Oktoba 21
Ahesabiwa rasmi katika zoezi la sensa nchini Afrika Kusini mwaka 2011
2011
Disemba
Asherehekea sikukuu ya Krismas na familia yake kijijini Qunu
2012
Februari 25
Alazwa hospitali kutokana na maumizu. Atoka baada ya siku moja
2012
Julai 18
Asherehekea miaka 94 ya kuzaliwa akiwa na familia yake huko Qunu, Eastern Cape

Disemba 8
Alazwa hospitali

Disemba 26
Atolewa
2013
Januari 1
Asherehekea mwaka mpya na familia yake mjini Johannesburg

Machi 9 - 10
Hospital

Machi 27 - Aprili 6
Hospitali

Juni 8
Alazwa hospitali

Desemba 5
Afariki Dunia

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni