Alhamisi, 5 Desemba 2013


Pointi za Arsenal zamtesa Moyes



Kocha Wenger 

Kocha Mkuu wa Manchester United, David Moyes amesema moja ya mambo yanayomuumiza moyo kwa sasa ni kuona wameachwa kwa pointi nyingi na Arsenal ambao wanaongoza Ligi Kuu England.
Kabla ya mechi za jana usiku Jumatano, Manchester United ilikuwa nyuma kwa pointi tisa kuwafikia vinara Arsenal, ambao kwa sasa wanajinafasi kwenye usukani wa ligi hiyo.
Sare ya mabao 2-2 dhidi ya Tottenham Hotspur Jumapili iliyopita iliwatibulia Manchester United, wakati Arsenal iliendelea kuwasha moto ilipoichapa Cardiff City mabao 3-0.
“Tumepoteza pointi mbili. Kwenye mechi dhidi ya Tottenham unaweza kuona matokeo haya ni sawa, kwa sababu si timu nyepesi inapokuwa nyumbani. Lakini, kinachoumiza ni zile pointi tulizopoteza kwa Cardiff,” alisema Moyes.
“Kinachoniumiza ni kwamba tumeshindwa kuwakaribia Arsenal, lakini bado naamini msimu ni mrefu na chochote kinaweza kutokea. Bado kuna mechi nyingi sana. Nadhani Ligi Kuu ni ngumu sana, yatupasa tuendelee kupambana na nadhani tutakuwa kwenye nafasi nzuri kuanzia mwakani.”
Manchester United jana Jumatano usiku ilitarajia kumenyana na Everton kwenye Uwanja wa Old Trafford, wakati vinara Arsenal walikuwa Emirates kukipiga na Hull City

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni