TBL MBEYA
Akizungumza na waandishi wa, habari mratibu wa usalama na afya kazini wa TBL Mbeya Misana Misana alisema, wamechukua uamuzi wa kupima ukimwi ili kuhamasisha jamii kujitokeza kupimwa ugonjwa huo.
Alisema, ipo haja ya wananchi kuendelea kuhamasishwa kwa njia mbalimbali kupima afya zao kwa kuwa bado wapo ambao bado wanaogopa au kuona aibu kwenda kupimwa ukimwi kutokana na sababu mbalimbali.
"Hatua ya kujitokeza kwa wafanayakazi wa TBL Mbeya kupimwa itakuwa hamasa kubwa kwa watu wengine na pia itasaidia wafanyakazi wenyewe kutambua afya zao na hivyo kuchagua kwa usahihi aina ya maisha watakayoishi katika kupambana na ukimwi.
Na Mbeya yetu
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni