Thursday, April 18, 2013
NJIA ZA KUPATA MAFANIKIO. (
Njia Za Kupata Mafanikio
Na christopher ngaga
. Lakini kabla hujasoma huo muendelezo wa Njia Za Kupata Mafanikio napenda kukusalimia na kukukaribisha na pia kukushukuru kwa kuunga nami, sasa endelea
1. Kuwa na malengo/mitazamo au ndoto.
Washindi wanapata wanachohitaji kwasababu wanajua nini wanahitaji. Wana mitazamo ambayo inawahamasisha na inawapa nguvu kufikia malengo yao. Hivyo katika kuelekea katika mafanikio ni vyema kuwa na malengo ambayo malengo hayo yatahamasishwa na mitazamo chanya aliyonayo mtu binafsi.
2. Kuwa na shauku.
Katika kufikia malengo yako, hakikisha unayajengea shughuli ili kuweza kuyafikia. Hii ni njia sahihi katika kufikia malengo yako.
3. Ishi kwa ukweli.
Ukweli ni moja kati ya njia zinazoweza kukufanikishia malengo yako hivyo jenga tabia ya kuwa mkweli hasa katika jamii inayokuzunguka.
4. Kubali mabadiliko.
Kuwa mwepesi kukubali mabadiliko jenga tabia ya kuwa mwepesi kukubali na kupokea mabadiliko katika maisha yako. Hii pia itakusaidia kiafya katika kuondoamsongo wa mawazo. Pale unapokosea jikubali na kufanya mabadiliko.
5. Kuwa tayari kwa lolote.
Katika hatua ya kuelekea katika mafanikio ni vyema kuwa tayari kwa lolote litakalotokea hii itakusaidia hata pale unaposhindwa kufanikisha jambo fulani kuwa na moyo na utayari wa kuweza kusonga mbele.
6.Jenga mahusiano mazuri na watu wa aina tofautitofauti.
Hii itakusaidia kuweza kujifunza mambo mengi na tofautitofauti kutoka kwa watu hao ili kufikia malengo yako. Kwa kutumia mawazo/fikra zao na mtindo wa maisha waishio watu hao.
ZINGATIA:
Kuwa na malengo ya baadae katika maisha yako, weka jitihada katika kila unachokifanya, jiamini wewe mwenyewe kwanza ili na wengine wakuamini pia kwani bila ya kujiamini wewe wengine hawawezi kukuamini, linda/tunza muda wako kwa kuutumia vizuri, jitambue na ujione wewe ni mshindi na usife moyo changamoto katika maisha ndiyo njia ya mafanikio.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni