Jumapili, 29 Machi 2015

Huu ni udhaifu mkubwa wa kifikra.

SI HEKIMA! SI UUNGWANA! NI KUWATUKANA WATANZANIA .. NI KUITUKANA SERIKALI!
Na Jacob Malihoja
Intellectuals na viongozi wakubwa wanapoingia kwenye mkumbo wa kuhisi na kugeuza hisia kuwa ushahidi na kutuhumu wenzao ni aibu!.
===========================
Huu ni udhaifu mkubwa wa kifikra.
Kiongozi, wala Intellectual hawapaswi kutumia taarifa za kuhisi, taarifa za kimajungu kutoa shutuma. Sifa za intellectual na kiongozi makini ni pamoja na kuchambua linalomjia na kujaribu kutafuta vyanzo yakinifu kuhakiki mambo hasa linapokuja suala la shutuma kwa mtu yeyote. Tupo katika kipindi cha vita za kisiasa, sasa kiongozi unasikia jambo tu unakurupuka na kulalama na kutuhumu bila kutafakari kuwa taarifa hizi zaweza kuja kwangu na upepo wa upande gani, huo ni udhaifu uliopitiliza.

Nape Moses Mnauye, January Makamba, Livingstone Lusinde na wengine wenye mawazo yafananayo mngemwambia Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete aivunje TAKUKURU maana miaka nenda rudi mnalalama haijakamata tukio hata moja wakati nyinyi mnayajua na mnayaona, basi haina kazi ya kufanya. Au labda tuwaite nyinyi ni wazembe maana mnaona matukio hampeleki TAKUKURU yafanyiwe kazi.
Inaonekana nyinyi mna wataalamu wa kuona rushwa na michezo hiyo kuliko TAKUKURU, ama TAKUKURU miaka yote wanaona ila wameshindwa kazi. Ivunjeni .. Wekeni hao watu wenu wanaowaletea hizo taarifa mnazozitumia kushutumu wenzenu .. Maana hao ndio wanaoweza kazi.
Sheria inasema mwananchi ana haki ya kukamata .. Basi nendeni mkakamate nyinyi hayo matukio mnayolalama .. Mana TAKUKURU .. POLISI wameshindwa.. ..
Wenye Hekima wanashindwa kuwaelewa .. Miaka yote vyombo vizito vya kitaifa havija toa taarifa yoyote, havija lalamika .. Havijashuhudia .. Ila nyinyi mna macho zaidi kujua hayo.. Ya kuona hayo .. Hizo taasisi mmeweka za nini .. Vunjeni kitengo cha Usalama wa Taifa, Vunjeni jeshi la polisi, vunjeni TAKUKURU .. Wekeni hao watu wenu wanaowaletea hizo taarifa maana ndio wanaweza kazi kuliko taasisi zote.
Kwa wenye hekima, watafiti na wachambuzi wa mambo kwa kina tunajua hakuna lingine linalowasukuma ni makundi, vita ya urais .. Mnaumizwa na kiwango kikubwa cha kukubalika kwa Edward Lowassa. Hivi mmeangalia maboriti kwenye macho yenu.. hivi ni mangapi mmefanya na mnafanya ..wengine walidiriki hata kuhamasisha kuanzisha chama cha kisiasa na kuchangia uanzishwaji wake nje ya CCM, wengine wamechapisha vitabu na mambo kadha wa kadha zikiwa ni kampeni za chini chini .. mbona maboriti hayo kwenye macho yenu hamyasemi.
Hivi ni nani aambiwe tunakuja kukutembelea akakaa kimya asiandae mapokezi ya wageni wake.. Hivi nyinyi kwenu mnapokuwa na wageni hamuandai kuwapokea? Au mtu anayetazamiwa kugombea urais anatakiwa kuwa kama ROBOT? Asicheke na watu, asishiriki na watu, asipokee wageni .. Wageni wakija waje kivyao .. Pengine wachungulie tu madirishani waondoke.
Mngewawekea kanuni ya kukataa wageni pia ili wasionekane wanafanya kampeni .. Mbona hamkuweka .. Nani ana tatizio hapo ..acheni kulalama .. Kwa tabia hiyo mnatufunulia kuwa ninyi ndio Wasaliti wakubwa wa CCM, Nyinyi ndio mnataka kukigawa chama .. nyinyi mko tayari CCM iwe Chama Cha upinzani lakini Lowassa asiende ikulu .. Wasaliti wakubwa wa Watanzania, Mnaitukana Serikali kwa Vyombo vyake kushindwa kazi na kujionesha nyinyi ndio mnaona maovu .. Wasaliti wakubwa wa umoja na mshikamano wa Chama Cha Mapinduzi. Mnawatukana mamilioni ya watanzania, wenye mapenzi kwa Lowassa eti wanalipwa kufanya hivyo,huo ni usaliti kwa watu wenu .. na mwisho mnamtukana Rais Dr. Jakaya Kikwete aliyehamasisha watu kama wanamwona mtu anaweza wakamshawishi.
Acheni wananchi, Acheni wana CCM waamue.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki CCM
Mungu Wabariki viongozi wa CCM na uwajaze hekima waache tabia ya Kugeuza hisia kuwa Ushahidi na kutengeneza tuhuma.

source   Jacob Malihoja facebook page

TANZANIA NCHI YANGU:

......One of the cardinal principles of Economics is Opportunity Cost. Do the fast thing first, and those which can wait let them wait.....
Hebu tujaribu kufanya hesabu ndogo za kugawanya na kuzidisha za darasa la tano. Ni hivi, wabunge wawili walioteuliwa watalipwa mishahara ya miezi mitano bure maana hatutegemei jipya watakalolifanya huko bungeni. Mshahara kwa mbunge mmoja ni Mil.11 mara miezi mitano watakayofanya kazi ni jumla ya Sh.Mil 55 kwa kila mmoja. Kwa wote wawili ni Mil.110.
Wabunge hawa walioteuliwa leo watalipwa kiinua mgongo kwa viwango vya wabunge wa kawaida Sh.Mil.90 kila mmoja ifikapo tar.31 mwezi July mwaka huu. Kwa wote wawili ni Mil.180.
Taarifa ya Ikulu inasema uteuzi wao unaanza tarehe 20, hivyo basi kuanzia tar.21 wataanza kulipwa posho za vikao vya bunge kwa siku 10 zilizobakia kwenye bunge hili linaloendelea. Posho ya siku moja ni Sh.330,000/= kwa siku kumi ni Mil.3 na laki 3.
Kwenye bunge la bajeti Watalipwa posho ya 330,000/= kwa siku. Bunge hilo litatumia jumla ya siku 60. Hivyo mbunge mmoja atalipwa Mil.19 na laki 8, kwa muda wote wa bunge la bajeti. Kwa wote wawili watalipwa mil.39 na laki 6.
Wabunge hawa "watakopeshwa" magari ya kifahari ya kutembelea. Yani kama walikua wakitumia usafiri wa umma, kuanzia tar.20 March wameambiwa stop. Watapanda Mashangingi yanayokadiriwa kugharimu Mil.120 kwa moja, kwa wote wawili ni Mil.240.
Kwa ujumla makadirio ya gharama zote za wabunge hawa wawili kwa miezi mitano tu watakayofanya kazi watatumia jumla ya Shilingi Milioni 573 na laki 2.
Pesa hizi zinatosha kulipia mikopo ya elimu ya juu kwa semester moja kwa wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza Chuo kikuu cha St.Augustine, au Chuo Kikuu Dodoma kwa wanafunzi wanaosoma Social Science.
Pia pesa hizi zingeweza kujenga maabara za kisasa katika shule 12 Tanzania. Zingeweza kulipa mishahara ya waalimu (daraja la pili) 1,432 wa shule mbalimbali za sekondari nchini. Pia fedha hizi zingeweza kutolewa kama mkopo kwa vijana wanaohitimu vyuo vya Elimu ya juu nchini na kukosa ajira. Jumla ya vijana 573 wangenufaika kwa mkopo wa Mil.1 kila mmoja.
Lakini cha ajabu pesa zote hizi zitatumiwa na wabunge wawili tu tena kwa kipindi cha miezi mitano tu, with no expectation of return. Hatutegemei wabunge hawa watafanya lolote jipya huko bungeni litakalogharimu hizo Mil.573 watakazotumia.
Kwa lugha rahisi ni kuwa hatutegemei output ya wabunge hawa izidi input. Hakuna mbunge yeyote atakayeweza kutoa hoja zitakazo-value hizo Mil.573 watakazotumia, hata wakisaidiwa na huyo aliyewateua.
Sasa nimejiuliza, hivi katika mazingira haya ambayo hatuna rasilimali za kutosha kulinganisha na mahitaji tuliyonayo, je kulikua na ulazima wowote wa kuteua wabunge hao?
Tunahitaji pesa za kujenga maabara, kujenga shule, kulipia wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu mikopo, kulipa mishahara, kununua madawa etc. Lakini tumeacha vyote hivyo tumetoa kipaumbele kwa wabunge tena wa kuteuliwa.
Tafakri......