Miji mikubwa miwili ya Brazil,Sao Paulo na Rio de Janeiro imetengua upandishaji wa nauli kwa usafiri wa umma.
Uamuzi huo unakidhi dai muhimu la waandamanaji ambao wamekuwa wakiaandamana katika maandamano makubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa katika nchi hiyo kwa miaka ishirini. Gavana wa jimbo la Sao Paulo Geraldo Alckmin amesema hapo jana anatumai hatua hiyo ya kubatilisha ongezeko la gharama za usafiri itarudisha utulivu unaohitajika ili kujadili masuala hayo kwa utulivu.Brazil imekumbwa na maandamano tokea wiki iliopita wakati watu walipoingia barabarani katika mji wa Sao Paulo kupinga ongezeko la nauli za mabasi na treni. Mitandao ya kijamii ilisaidia kuyageuza maandamano hayo kuwa vuguvugu la nchi nzima ambapo hapo Jumatatu zaidi ya waandamanaji 200,000 walijitokeza nchini kote Brazil na kutanuwa kilio chao kutoka suala la nauli na kujumuisha rushwa na gharama kubwa zinazotumika kwa maandalizi ya michuano ya soka Kombe la Dunia mwaka 2014.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni