Alhamisi, 20 Juni 2013

Urusi na China wahusika wakuu kusafirisha binaadamu kwa magendo

Ripoti ya kila mwaka inayotolewa na serikali ya Marekani hapo jana imeitaja China na Urusi ni miongoni mwa wakiukaji wakubwa kabisa katika mapambano ya kupiga vita kutumikishwa watu kwa nguvu na kusafirishwa binaadamu kwa ajili ya biashara ya ngono.
Ripoti hiyo imesema Urusi imeshindwa kutowa ulinzi kwa wahanga wa biashara ya kusafirisha binaadamu. Imesema China haikuchukuwa hatua kubwa za kupiga marufuku aina zote za usafirishaji wa binaadamu kwa magendo na kuwaadhibu wahusika. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani katika repoti yake hiyo huziorodhesha nchi kwa mujibu wa juhudi zao za kupambana na usafirishaji wa binaadamu kinyume na sheria.
Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imetowa taarifa inayosema ripoti hiyo imetumia utaratibu usiokubalika kwa kuziweka nchi kwa mujibu zinavyojipendekeza kwa serikali ya Marekani.
  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni