Fanya afya kipaumbele chako na siyo madawa ya kulevya, ni ujumbe
mahsusi wa Umoja wa Mataifa hii leo ambayo ni siku ya kimataifa dhidi ya
matumizi na usafirishaji wa madawa ya kulevya. Ripoti ya Flora Nducha
inafafanua zaidi.(Ripoti ya Flora)
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kudhibiti madawa ya kulevya na uhalifu
UNODC inaeleza bayana kuwa matumizi ya madawa yanaharibu afya na ustawi
wa binadamu huku ikionyesha wasiwasi kutokana na kuibuka kwa tatizo
jipya la ongezeko la mahitaji ya madawa yasiyo chini ya udhibiti wa
kimataifa ambayo huchanganywa na watumiaji hulewa, madawa ambayo ni
tofauti na yale yaliyozoeleka ambayo ni Cocaine, Heroine na bangi.
Mkuu wa maabara ya kisayansi ya UNODC Justice Tettey anasema kuwa
madawa hayo yanauzwa kihalali kabisa lakini mchanganyiko wake hujipatia
majina ya mtaani kama vile SPICE au Meow-Meow na vijana kudhani kuwa
hayana madhara.
(SAUTI YA Tettey)
Fatma Musa Juma ni mmiliki wa moja ya makazi ya kusaidia watumiaji wa
madawa ya kulevya huko Tanzania Zanzibar kurejea katika maisha ya
kawaida. Je vijana hupataje fedha za kununua madawa hayo?
(SAUTI YA FATMA)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni