Wakati
Muungano wa nchi za Afrika (AU) unapoanza mkutano wake wa 21 na
kuadhimisha miaka 50 ya kuungana kwa bara Afrika, Mpango wa pamoja wa
Umoja wa Mataifa kuhusu virusi vya HIV na UKIMWI (UNAIDS), umetoa ripoti
mpya inayoonyesha hatua zilizopigwa katika kupiga vita UKIMWI barani
humo.
Kwa
mujibu wa ripoti hiyo, idadi ya watu wanaopokea matibabu ya dawa za
kupunguza makali ya virusi vya HIV imeongezeka na kufikia milioni 7.1
mwaka 2012, wakati idadi hiyo ilikuwa chini ya milioni 1 mnamo mwaka
2005. Mwaka uliopita pekee, idadi hiyo ilipanda kwa watu milioni moja.
Kwa
mujibu wa ripoti hiyo ya UNAIDS, vifo kutokana na UKIMWI pia
vimeendelea kupungua- viwango vya vifo vikishuka kwa asilimia 32 kati ya
2005 na 2011, huku viwango vya maambukizi mapya ya virusi vya HIV
vikishuka kwa asilimia 33 kati ya 2001 na 2011.
Ripoti
hiyo inasema ufanisi huu umetokana na uongozi imara na wajibu wa
ushirikiano barani Afrika na katika jamii ya kimataifa, huku ikitoa wito
kuwepo juhudi endelevu ili kuhakikisha bara Afrika linafikia lengo la
kutokomeza maambukizi, ubaguzi na vifo vitokananvyo na UKIMWI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni