Alhamisi, 6 Juni 2013

Janga la Elimu Tanzania!!!

Janga La Elimu Tanzania: Tulikosea Wapi?
Licha ya kusifikia kama kisiwa cha amani na utulivu, Tanzania ni Taifa la Majanga ya Kila Aina. Kwa miaka zaidi ya hamsini sasa, bado tunapambana na maadui wale wale wa maendeleo – Umaskini, Ujinga na Maradhi huku pakiwa na dalili zote kwamba tumeishiwa silaha na na mbinu za kivita kukabiliana na maadui hawa watatu. Mada yangu ya leo itajikita zaidi katika janga la elimu ambalo ndio chimbuko wa adui ‘ujinga’. Janga la elimu ni suala linalotawala mijadala mingi kwa muda mrefu nchini, lakini kwa muda mrefu, viongozi walikuwa wanaendesha shughuli zao kama vile mfumo wa elimu ulikuwa hauna tatizo lolote.

Mjadala wetu utakuwa na tija zaidi iwapo utajikita katika kutafuta majibu kwa maswali makuu muhimu yafuatayo:


  1. Je, mfumo wetu wa elimu umekumbwa na tatizo gani?
  2. Je, ni wapi tulikosea huko nyuma (chini ya Ujamaa)?
  3. Je, mfumo wetu wa elimu unalipeleka wapi taifa letu (chini ya uliberali)?
  4. Nini kifanyike kuokoa taifa letu na janga hili?


Majibu kwa maswali haya yanahitaji utafiti wa kina, ila ni bahati mbaya sana, binafsi sijawahi kusoma utafiti wa aina hii popote, hasa utafiti uliotokana na juhudi zetu wenyewe kama taifa; Lakini kukosekana kwa utafiti wa namna hii haiwezi kutuzuia watanzania wenye mapenzi na pia nia njema na taifa letu kujadili suala hili, hasa ikiwa lengo ni kubadilishana mawazo juu ya ufumbuzi. Katika bandiko langu la kwanza, nitajadili Swali la Kwanza na la Pili (rejea hapo juu). Swali la tatu na la nne nitayajadili katika bandiko lingine ili kuepuka kuweka bandiko moja refu.

Historia ya nchi yetu inatuonyesha kwamba mara tu baada ya uhuru wa Tanganyika (1961), motivation na drive for education ilikuwa ni ya juu sana; Kwa mfano, ndani ya kipindi cha miaka kumi ya mwanzo ya uhuru, sekta ya elimu nchini ilikuwa kwa kasi kubwa – idadi ya shule iliongezeka, chuo kikuu cha DSM kilipanuliwa zaidi kutoka kuwa chuo chenye idara moja na kuwa chuo chenye idara nyingi zaidi, taasisi mbalimbali za elimu ya juu, ufundi, utafiti n.k, pia zilianzishwa. Lakini haikuchukua muda mrefu kabla ya sekta yetu ya elimu kuanza kukumbwa na msukosuko kama nitakavyojadili hapo chini:

Kwanza, Serikali ilifanya kosa kubwa la kuwa na utamaduni wa kutenga fedha kidogo sana kwenye bajeti kwa ajili ya Sekta ya elimu, hasa katika mazingira ambayo kasi ya ongezeko la watu nchini (population growth) ikiwa ni kubwa mno (i.e. tangia uhuru, wastani wa kasi ya ongezeko la watu imekuwa takribani 3%); Kwa mfano, bajeti kwa ajili ya Sekta ya Elimu haikuwa inazidi 10% - 12% kila mwaka; Katika kipindi hicho hicho, takwimu zinaonyesha kwamba serikali na taasisi zake mbalimbali zilikuwa zikitengewa mafungu makubwa sana tofauti na sekta ya elimu.

Pili, Administration ya Sekta ya elimu ikawa very centralized, na mbaya zaidi local authorities zikafutwa suala ambalo lilipelekea shule nyingi zilizokuwa zikiendeshwa na town councils kupotea; Ni katika kipindi hiki pia shule nyingi ambazo zilikuwa chini ya NGOs zikataifishwa na serikali; Masuala haya yakapelekea faida na hasara kadhaa. Tukianza na faida, kubwa kuliko zote ilikuwa ni integration of religious and racially segregated schools; Tukija upande wa hasara, kubwa kuliko zote ni kwamba centralization ya mfumo wa elimu ulipelekea de-professionalization of the teaching profession in Tanzania. A quick cost – benefit analysis katika suala hili utaonyesha kwamba madhara yalikuwa ni makubwa kuliko faida; Pigo takatifu kwa mfumo wetu wa elimu ilikuwa pale working & material conditions za walimu zilipoanzwa kuwa neglected na serikali; Ni katika kipindi hicho taifa likashuhudia jinsi gani ‘teaching profession’ ikaanza kuwa downgraded & degraded – both socially and materially huku professions nyingine zikianza kuwa upgraded zaidi. Kwa mfano, ilifikia hatua kwamba – kama mtu unataka kuwa wa maana katika jamii, basi ilikuwa hauna budi uwe mwana siasa wa CCM; Lakini pia iwapo mtu ulikuwa unataka kuboresha maisha yako kiuchumi, basi ilikuwa hauna budi uwe katika shirika la umma; Na huu ndio ukawa mwanza wa exodus ya professional teachers kuhamia kwenye siasa na mashirika ya umma; Kwa mfano, kuanzia miaka ya sabini, nafasi za utendaji serikalini, mashirika mengi ya umma (pamoja na viwanda vingi) yalianza kujaa maafisa wengi sana wenye background ya ualimu. Sababu za msingi juu ya hili haikuwa nyingine zaidi ya wahusika kutafuta maisha bora zaidi i.e. profession nje ya ualimu offered better material incentives;

Je, matokeo yake yakawa nini?


  • Kwanza, ubora/Viwango vya ufundishaji ukaanza kuporomoka (deterioration of quality of instructions);
  • Pili, ethics (maadili) katika sekta ya elimu yakaanza kuporomoka;
  • Tatu, fani ya ualimu ikaanza kugeuka kuwa biashara ambapo sasa walimu wengi wakaanzisha ‘Tuitions’ pembeni;


Pamoja na yote haya, response ya serikali haikuwa katika kuboresha sekta ya elimu, hasa kwa kuongeza allocation ya budget kwa ajili ya sekta ya elimu; In summary – the government got its priorities wrong, na the society got its social values wrong; Na haya mawili ya mahusiano makubwa sana kama ambavyo tutakuja jadiili baadae;

Kuna hoja zinajengwa kwamba ni muhimu janga la elimu pia likajadiliwa katika muktadha wa uchumi, hasa kwa kuzingatia mgogoro wa kiuchumi nchini katika kipindi cha miaka ya sabini na themanini; Pamoja na ukweli kwamba mgogoro huu ulichangia katika janga la elimu nchini, kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu kulaumu kila mapungufu yanayojitokeza nchini kwamba ni kwa sababu ya ujamaa (azimio la Arusha), huku wahusika wakijenga hoja kwamba mwarubaini wa matatizo/majanga yote katika taifa letu ni mfumo wa uliberali na soko huria; Swali langu kwa watu hawa ni:


  • Je, Wakati wa ujamaa, kulikuwa na chochote ndani ya azimio la Arusha kilichozuia serikali kuipa sekta ya elimu kipaumbele katika bajeti?
  • Je, Azimio la Arusha lilitukataza kuwathamini walimu na badala yake kuhimiza kuwathamini viongozi wa chama na serikali, morally & materially?


Nitarejea kujadili swali la tatu na nne nililyoainisha hapo juu i.e:


  1. Je, mfumo wetu wa elimu unalipeleka wapi taifa letu (chini ya uliberali)?
  2. Nini kifanyike kuokoa taifa letu na janga hili?
Kwanza kabisa pawepo na sera ya elimu ambayo inaeleweka na ambayo itasimamiwa.na watu weledi na wala siyo washabiki wa siasa. Mtu anayeweza kuielewa sera na kuitafsiri. Ebu tuelezane. Hivi sasa hivi mfumo wa elimu unamwandaa Mtanzania wa namna gani? Is anybody interested to know? Kids are just going to school and come out unlearned. What is the aftermath? (Tushilikiane kuitokomeza)

"In the future, it is possible that a Second Party will grow in Tanganyika, but in one sense such a growth would represent a failure by TANU."

J.K Nyerere, 1968.


ALIPATA division II sasa AMEKUWA TANZANIA ONE
Mwanafunzi bora wa kwanza kitaifa katika matokeo yaliyorekebishwa ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka 2012, Said Irando kutoka Shule ya Sekondari Feza ya jijini Dar es Salaam, ameeleza kushangazwa na matokeo hayo kwa kuwa hakuyatarajia.
Mwanafunzi huyo ambaye tayari ameshaanza masomo ya Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari Feza, alisema kuwa ingawa alisoma kwa bidii lakini hakudhani kama angeweza kushika nafasi ya kwanza kitaifa na kwamba anamini mafanikio yake kitaaluma yana ‘mkono wa Mungu’.

“Sikutegemea kabisa kuwa mwanafunzi bora, ingawa nilisoma kwa bidii kubwa nia yangu ilikuwa ni kutaka kufaulu tu; Ni Mungu amenisaidia,” alisema Irando.

Alisema kujituma katika masomo, mazingira mazuri ya kusomea na upatikanaji wa vifaa muhimu vya kujifunzia ndiyo yaliyomwezesha kusoma na kufanya vizuri.



Irando ambaye ni mtoto wa kwanza katika familia yenye watoto watatu, alisema kurekebishwa kwa matokeo ya kidato cha nne kulibadilisha alama za matokeo yake kutoka Daraja la kwanza akiwa na alama tisa hadi saba, zilizomfanya kuwa mwanafunzi bora kitaifa na mwafunzi bora wa kwanza kati ya wavulana kumi bora pia kitaifa.



Mwanafunzi huyo alibainisha kuwa pamoja na wazazi wake kuwa ni wafanyabiashara, yeye anatamani kuwa mhandisi ingawa bado hajajua atakuwa mhandisi katika tasnia gani.

“Natamani sana kuwa mhandisi hiyo ndiyo ndoto yangu ingawa bado sijajua nitakuwa mhandisi wa sekta gani,” alisema Irando.



Irando alisoma elimu ya msingi katika Shule ya Msingi J.K Nyerere ambako alifaulu na kuchaguliwa kujiunga na Sekondari Pugu, lakini wazazi wake waliamua kumpeleka Shule ya Sekondari Feza.

Naye mwanafunzi Joshua Azza kutoka Sekondari ya Wavulana Marian ambaye ameshika nafasi ya saba kitaifa kati ya wanafunzi kumi bora baada ya kupata daraja la kwanza akiwa na alama 11, alisema ameyapokea matokeo hayo kwa furaha akiamini atatimiza lengo lake la kuwa daktari wa upasuaji.



“Natarajia kuwa daktari wa upasuaji, kwa matokeo haya nadhani nitafanikiwa,” alisema Azza ambaye wazazi wake wote ni walimu alipozungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Saidi Nchimbi kutoka Sekondari ya Feza, ambaye ameshika nafasi ya nane kati ya wanafunzi kumi bora kitaifa, alisema kuwa siku zote alikuwa akisoma kwa uwezo wake wote na kwamba alikuwa akitamani kufaulu kwenye mitihani yake yote aliyopewa.

Nchimbi amefanikiwa kushika nafasi hiyo baada ya kupata daraja la kwanza akiwa na alama nane. Katika matokeo ya awali mwanafunzi huyo alikuwa na alama 11.

NAFASI
NAMBA
JINA
JINSI
JINA LA SHULE NA MKOA
1
S0189-0063SAID JUMA IRANDO
M
FEZA BOYS' S S (DAR ES SALAAM)
2
S4459-0028ALEX ELIFAS
M
JUDE MOSHONO S S (ARUSHA)
3
S0189-0039JASPER GEOPHREY KAJIRU
M
FEZA BOYS' S S (DAR ES SALAAM)
4
S2549-0086MOSES J BOSCO
M
ALPHA SECONDARY S S (DAR ES SALAAM)
5
S4213-0074YOHANA L MAYENGA
M
MARIAN BOYS' S S (PWANI)
6
S0239-0072NGUSE NGULUMBI
F
ST. FRANCIS GIRLS S S (MBEYA)
7
S4213-0044JOSHUA Z AZZA
M
MARIAN BOYS' S S (PWANI)
8
S0189-0062SAID ATWAYA NCHIMBI
M
FEZA BOYS' S S (DAR ES SALAAM)
9
S0867-0134LUPYANA L KINYAMAGOHA
M
PANDAHILL S S (MBEYA)
10
S0101-0350PETER SEREKA KICHOGO
NAFASI
NAMBA
JINA
JINSI
JINA LA SHULE NA MKOA
1
S0189-0063SAID JUMA IRANDO
M
FEZA BOYS' S S (DAR ES SALAAM)
2
S4459-0028ALEX ELIFAS
M
JUDE MOSHONO S S (ARUSHA)
3
S0189-0039JASPER GEOPHREY KAJIRU
M
FEZA BOYS' S S (DAR ES SALAAM)
4
S2549-0086MOSES J BOSCO
M
ALPHA SECONDARY S S (DAR ES SALAAM)
5
S4213-0074YOHANA L MAYENGA
M
MARIAN BOYS' S S (PWANI)
6
S0239-0072NGUSE NGULUMBI
F
ST. FRANCIS GIRLS S S (MBEYA)
7
S4213-0044JOSHUA Z AZZA
M
MARIAN BOYS' S S (PWANI)
8
S0189-0062SAID ATWAYA NCHIMBI
M
FEZA BOYS' S S (DAR ES SALAAM)
9
S0867-0134LUPYANA L KINYAMAGOHA
M
PANDAHILL S S (MBEYA)
10
S0101-0350PETER SEREKA KICHOGO
M
AZANIA S S (DAR ES SALAAM)
source mwananchi na Necta

Kweli hii ndo necta dah..... Siamini!!!!
Wakuu jf mi ni mojawapo ya wanafunzi waliofaulu kwenda form v 2013 kabla ya matokeo "kufutwa lakin cha kushangaza matokeo yangu hayajabadilika wakati kuna watu walokuwa na iv za 28 na 27 lakini wamepanda hadi 25 na 24 alafu mimi nimebaki palepale 25 inakuwaje siamini au wamekosea nini?
Mawazo wakuu hapo ndo sijawaelewa necta kabisaaaaa"  alisikika kijana mmoja akilalamika...............

Kufutwa kwa matokeo
Mimi kwa jina naitwa Yassin Said Athumani, nikijana ninaeishi morogoro na ni mmoja kati yawanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne katika shule ya Jabal hiraa seminary school lakini matokeo yangu yalifutwa na BARAZA LA MITIHANITANZANIA kwa madai kuwa katika majibu yangu somo moja la mwisho ambalo ni computer studies (plactical) kua mimi na wenzangu wanne tumetumia takwimu sio sahihi...

 Hvyo basi niuzembe ambao ulifanywa na wasimamizi pamojana mwanafunzi mmoja na mwalim wetu wa somo pale shuleni... mwalim huyo wakishirikiana namwanafunzi walipewa fursa ya kuchukua flash disk na kukusanya majibu yetu yote ambao siou taratibu na sheria za mitihani.

 Basi walitumia nafasi hiyo kuhamisha majibu yangu na kuwekewa wale wengine kwa sababu walijua uwezo
wangu ktk hilo somo hapo shuleni na kuwafanya BARAZA KUFUTA MATOKEO YANGU NA YAO PIA...
Nilipeleka malalamiko hayo pale baraza la mitihani na baada ya siku kadhaa mbele TUME ilioundwa
na WAZIRI MKUU ilikuja pale shuleni na kutuhoji juu ya yale yaliotokea pale shuleni lakini baada ya
matokeo yoote kufutwa na kuyapanga upya basi namimi nilipata matumaini kuwa huenda na yangu
yakatoka ila sikuyaona roho inaniuma nina majonzi sina wa kunisomesha tena kwa shida niliopata kusoma kidato cha kwanza mpaka cha nne kwashida na tabu kubwa

NINAOMBA MSAADA WAKO WA KISHERIA AU
KAWAIDA TU NIFANYE NINI ILI BARAZA LA
MITIHANI WAWEZE KUNIPA MATOKEO YANGU NA
KUWAPA ADHABU WALE WOOTE WALIOHUSIKA JUU
YA HILI
YASSIN SAID ATHUMANI
0719715947

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni