Katiba Tanzania Bara yanukia

Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe
Na mussa_2014 blog
Kwa ufupi
- "Watu wasiwe na hofu. Sioni tatizo endapo rasimu itapita bila mabadiliko na kupata Katiba Mpya. Aprili mwakani mpaka Desemba inatosha kabisa kuandaa Katiba ya Tanzania Bara na tukaenda katika Uchaguzi Mkuu tukiwa na Katiba Mpya".
Chikawe alizungumza Dar es Salaam jana kuwa, ikiwa mchakato wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano utakamilika kama inavyokusudiwa na rasimu hiyo kupitishwa na wananchi katika ngazi zote bila mabadiliko, muda utakaobaki utatosha kuandaa Katiba ya Tanzania Bara.
“Watu wasiwe na hofu. Sioni tatizo endapo rasimu itapita bila mabadiliko na kupata Katiba Mpya. Aprili mwakani mpaka Desemba inatosha kabisa kuandaa Katiba ya Tanzania Bara na tukaenda katika Uchaguzi Mkuu tukiwa na Katiba Mpya,” alisema na kuongeza:
“Tunaweza kuwatumia wajumbe walewale wa Tume ya Katiba, lakini safari hii tukawachukua wale wa Tanzania Bara pekee wakashiriki katika kuandaa Katiba hiyo.”
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
Wakati Chikawe akitoa kauli hiyo, habari kutoka ndani ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), zinasema kutokana na mapendekezo ya kuwapo kwa Serikali tatu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema anaandaa “kitu muhimu” ambacho atakiwasilisha bungeni siku chache zijazo.
Ndugai apinga Spika kutokuwa mbunge

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amepinga
Na mussa_2014 blog
Kwa ufupi
- Hivi kweli, kuna umoja wa madaktari, halafu kiongozi wao atoke nje ya fani ya udaktari, sidhani kama kutakuwa na ufanisi na kuelewana hapo
Ndugai, ambaye ni Mbunge wa Kongwa aliiambia Mwananchi jana kuwa ni kitu kizuri kwa Spika kuwa miongoni mwa wabunge. “Mimi nadhani kuna tatizo hapa. Pamoja na kwamba ni rasimu, lakini ni kosa kwa Spika kutokuwa na chama.
“Hivi kweli, kuna umoja wa madaktari, halafu kiongozi wao atoke nje ya fani ya udaktari, sidhani kama kutakuwa na ufanisi na kuelewana hapo,” aliongeza Ndugai.Hata hivyo, Ndugai alisema kuwa suala zima ni mapendekezo, na litakuja hadi Bungeni kwa majadiliano na hii itapata changamoto nyingi.
Akitoa mawazo yake kuhusu rasimu, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Grace Kiwelu alisema anaamini hatua hiyop itaongeza uwajibikaji.
“Mawaziri wengine walikuwa wamejisahau na kuwakandamiza wale waliotakiwa kuwahudumia kwa visingizo kuwa ni kambi za upinzani,” alisema Naye Profesa Juma Kapuya, ambaye ni Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM), alionya kitendo cha Mawaziri kwamba wasitokane na Bunge.
kitasababisha wasomi kutowania nafasi hiyo.
“Kwa sasa wengi wanapigania ubunge wakiangalia kupata uwaziri, sasa kutenganisha haya ni wazi wataibuka wabunge wasio na ubora kwa kuwa hakuna motisha mbele,” alifafanua
MICHEZO/SPORTS
‘Yanga, Simba acheni siasa’

Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Nicholaus Musonye
Akizungumza, Musonye alisema Baraza lake lina barua rasmi kutoka Serikali ya Sudan ikiwahakikishia hali ya usalama kwa timu zote ambazo zitakwenda na kudai kuwa iwapo Simba na Yanga hazitaenda sheria ipo wazi na klabu hizo zinaijua.
“Nimetoka huko Sudan juzi, nimekaa karibu siku 14 sijaona machafuko yoyote, hayo mnayosema ni fitina tu ili mashindano yasifanyike kule, na Simba na Yanga zisishawishike kuacha kuja, tunaamini zimejiandaa vizuri kwa mashindano ya mwaka huu.”
“Hata hivyo hatuzilazimishi kushiriki kama watasikiliza Serikali yao, sisi sheria zetu zipo wazi na wanazifahamu, kwa sasa siwezi kusema ni hatua gani tutawachukulia wasipoleta timu kwa sababu bado hawajatuambia rasmi hawashiriki.,”alisema Musonye.
Kwa mujibu wa sheria za Cecafa timu ikijitoa kwenye mashindano itafungiwa siyo chini ya miaka miwili kushiriki michuano ya bBaraza hilo.
Kauli ya Musonye imekuja ikiwa ni siku mbili baada ya Waziri Membe kusema amesikitishwa na Cecafa kuamua kupeleka michuano hiyo huko bila ya ushauri wa Serikali na kwamba atafutilia kwa undani suala hilo na ikiwezekana kuzizuia Simba na Yanga kwenda kushiriki mashindano hayo ya Darfur.
“Mashindano haya ni makubwa sana katika uUkanda huu, Cecafa tupo makini sana na hali hiyo na ndiyo maana tumeamua kufanyia huko, kama Darfur kusingekuwa salama, sisi tusingekubali maombi yao, lakini tunajua ni salama na ndiyo maana tumeamua kuruhusu kufanyika huko,” alisema Musonye.
Musonye alisema kuwa wao wanajua nini maana ya vita na kamwe wasingeweza kuyapeleka mashindano hayo kwenye eneo ambalo halina amani na kutishia maisha ya wachezaji na viongozi.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Soka cha Sudan, Magdi Shams Eldin amesema kuwa taarifa kuwa hali si shwari katika miji hiyo siyo za kweli na kuwahakikisha kuwa kuna usalama wa hali ya juu.
Eldin alisema kuwa wameamua kufanyia mashindano hayo kwenye majimbo hayo ili kuondoa fikra hizo na kusema kuwa kuna mazingira mazuri na usalama wa hali ya juu.
Katika hatua nyingine, Musonye alikumbushia ahadi iliyotolewa na viongozi wa Yanga jijini Kigali mwaka jana waliponyakuwa ubingwa huo.
“Viongozi wa Yanga walipokwenda Rwanda walidai wataongeza dola 20,000 tunaisubiri na tumeshawandikia barua kuwakumbusha ili tuweze kupanga zawadi za washindi,”alisema Musonye.

Jose Mourinho 'targets Champions League glory at Chelsea'
Former Chelsea midfielder Alexei Smertin says Jose Mourinho has returned to Stamford Bridge to win the Champions League which eluded him during his first spell in charge of the Blues. | Mourinho led C... (photo: AP / Andres Kudacki)


Sky Bet offer a range of Mourinho specials upon his return to the Premier League


Neymar, Barcelona’s New Idol, Pledges Allegiance to Messi
BARCELONA, Spain — His arrival was orchestrated as if he were some blend of rock star and head of state, a 21-year-old object of adoration flown in from Brazil to the d... (photo: AP / Manu Fernandez)

Gattuso to coach relegated Palermo next season
June 3 (Reuters) - Former Italy and AC Milan hard man Gennaro Gattuso will coach Palermo in Serie B next season, club president Maurizio Zamparini said on Monday. | "I li... (photo: AP / Luca Bruno)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni