Jumatano, 5 Juni 2013

R.I.P. ALBERT MANGWEA

 

HIVI NDIVYO SHUGHULI NZIMA YA KUUPOKEA MWILI WA ALBERT MANGWEA ILIVYOKUWA LEO

Safari ilianzia Leaders Club - Hapa Gari la kubebea mwili wa Albert Mangwea likiwa tayari kwa safari ya kwenda Airport

Mabaga Fresh na Lamar wakijiandaa na safari ya kwenda kupokea mwili

Juma Nature

Inspekta Haroun na DJ Nelly wakisalimiana na Aneth Kushaba


TID na Jay Moe

Wasanii wakiwa kwenye vazi rasmi la msiba wa Albert Mangwea


Jay Dee

Baadhi ya wanandugu wa Magwair wakiwa wanasubiri mwili wa Albert Airport


Stamina, Quick Rocka na Izzo B wakiwa Airport wakisubiri mwili wa Albert utolewe

Banana Zorro


Wasanii mbalimbali wakiwa Airport tayari kuupokea mwili wa mpendwa wao Cow Obama Ngwea


Mchizi Mox

Joh Makini na Chege












Tuesday, June 4, 2013

MAANDALIZI YANAVYOENDELEA TAYARI KWA KUMUAGA ALBERT MANGWEA HAPO KESHO LEADERS CLUB




PICHA NA DJCHOKA BLOG
 
 

CRISTIANO RONALDO NJIANI KURUDI MANCHESTER?? AKATAA MKATABA MPYAMADRID, AUZA NYUMBA NA AKAUNTI YA UNITED TWITTER YAKAMRIBISHA TENA OT


Cristiano Ronaldo anaonekana kana kwamba yupo njiani kuondoka Real Madrid baada ya leo hii kutoka kwa taarifa kwamba mshambuliaji huyo wa kireno ameiweka sokoni nyumba yake ya kifahari anayoishi iliyopo jijini Madrid - Spain.

Kwa mujibu wa gazeti la AS ni kwamba Ronaldo ameiweka sokoni nyumba yake kwa dau la €5.4 million. Jumba hilo la kifahari lenye eneo la mita za mraba 800, huku likiwa na vyumba 7 vya kulalia, mabwawa mawili ya kuogelea na viwanja vya ukubwa wa mita 3,000.


Ronaldo amekuwa hafurahishwi na mbinu za utawala wa Raisi  Florentino Perez hasa kwenye suala lake la mkataba mpya, raisi huyo amekuwa akitumia suala la mkataba mpya wa Mreno huyo katika kuwafurahisha mashabiki kuliko mchezaji husika. Leo hii gazeti moja lenye habari za kuaminika la AS Bola la Ureno limeripoti kwamba Ronaldo amekataa kusaini mkataba mpya na Real unaoisha 2015.

David Gill, ambaye ni CEO anayemaliza muda wake Manchester United, mwezi uliopita alikutana na wakala wa Ronaldo Jorge Mendes jijini Madrid kuzungumzia kuhusu dili la kumrudisha Ronaldo Old Trafford wakati wa dirisha la usajili litakapofunguliwa.
 

BAADA YA FIGO, ZIDANE, BECKHAM, RONALDO NA KAKA - SASA FIORENTINO PEREZ ATHIBITISHA KWAMBA MADRID INAJIANDAA KUTUMA OFA KWA SPURS KUMNUNUA BALE

REAL MADRID jana usiku imetoa tamko rasmi kwa Tottenham: Tunakuja kumnunua Gareth Bale.

Raisi Florentino Perez alikiri kwa mara ya kwanza kwamba Real Madrid wapo tayari kumsaini Bale na akitoa ishara kwamba watatuma ofa ya kwanza siku chache zijazo. 

“Inabidi tukiboreshe kikosi chetu tena kwa umakini mkubwa - hilo litafanyika ndani wiki chache zijazo.”
Perez pia alikiri kwamba ameshakutana mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy mwaka jana kuzungumzia juu ya usajili wa Bale.

Aliongeza: "Bale ni mmoja ya wachezaji wakubwa barani ulaya na Real Madrid siku zote timu yetu imekuwa na wachezaji wakubwa wa soka.
"Nilikutana na mwenyekiti wa Tottenham mwaka jana na haki na majukumu ya kutetea maslahi ya timu yake.
"Kuhusu bei iliyozungumziwa kuhusu Bale, wachezaji hawana bei kubwa au ndogo - wao ni kama uwekezaji kwenye biashara ya soka.
"Wachezaji wenye gharama zaidi  ni wale ambao mara zote huwa ni uwekezaji kwenye biashara, na ikiwa watacheza vizuri basi lzima watengeneze faida kwenye uwekezaji huo."

Maneno ya Perez yanabeba uzito mkubwa ukizingatia ndio mtu aliyefanikisha dili kubwa kabisa kwenye historia ya soka duniani za usajili wa Luis Figo, Zinedine Zidane, David Beckham, Kaka na Cristiano Ronaldo.

TAIFA STARS YAWASILI SALAMA MOROCCO - TAYARI KUWAKANDAMIZA WAARABU JUMAMOSI

Taifa Stars imewasili hapa Marrakech, Morocco leo- Juni 3 mwaka huu tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji Morocco itakayochezwa Jumamosi- Juni 8 mwaka huu.
 
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia hoteli ya Pullman ambayo pia Ivory Coast ilifikia ilipokuja kucheza hapa dhidi ya Morocco. Stars imetua na wachezaji 21 huku Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu waliokuwa Maputo, Msumbiji kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho na timu yao ya TP Mazembe watawasili kesho- Juni 4 mwaka huu saa 8 mchana.
 
Taarifa na Afisa Habari wa TFF Boniface Wambura
 
Mechi kati ya Stars na Morocco itachezwa kuanzia saa 3 usiku kwa saa za hapa wakati nyumbani itakuwa ni saa 5 usiku.
Neymar Da Silva akiingia rasmi Camp Nou baada ya kufaulu vipimo leo hii na kujiunga na Barcelona kwa mkataba wa miaka mitano.


Arrival: Neymar was unveiled as a Barcelona player at the Nou Camp on Monday

Akisaini mkataba na Rais wa Barcelona Sandro Rosell


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni