Jumatatu, 10 Juni 2013

Kivumbi CCM

Mtanzania



Jumatatu, Juni 10, 2013 07:27 Na Bakari kimwanga, Dar es Salaam .*Kamati Kuu yakutana kujadili rasimu ya Katiba

*Hoja ya Serikali tatu kutawala mjadala

*Dk. Chegeni, Lipumba watoa msimamo mkali



Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete

KIVUMBI cha majadiliano ya Rasimu ya Katiba mpya, kinatarajia kutimka leo, wakati Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC), itakapokutana mjini Dar es Salaam kupitia mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wiki iliyopita.



Habari za kuaminika zilizopatikana mjini Dar es Salaam jana na kuthibitishwa na uongozi wa juu wa CCM, zinasema kikao hicho kitaongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.



“Ndugu kesho (leo), CCM inakutana chini ya Mwenyekiti wake Rais Kikwete na moja ya mada kubwa ambayo inaweza kutawala kikao hiki, ni pendekezo la kuunda Serikali tatu kama ilivyotolewa na Jaji Joseph Warioba (Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni